UTOTO WA MTANGAZAJI KIBONDE WAMCHUKIZA KAMANDA KOVA,NI KUHUSU PANYA ROAD AMVAA NA AMWAMBIA HAYA SOMA HAPA
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM YA DARESALAAM, AKIONYESHA PICHA ZA VIONGOZI WA PANYA ROAD KATIKA KIKAO CHAKE NA WAANDISHI WA HABARI MAPEMA HII LEO, KATIKA KIKAO HIHO KOVA AMESEMA TAYARI JUMLA YA PANYA ROAD 510 WAMEKAMATWA PAMOJA NA VIONGOZI WAO |
KILE
kinachoonekana watu wameanza kuchoka na Vituko vyake pamoja na Visa anavyofanya
Mtangazaji Maarufu wa redio ya Clauds Fm Eprahim Kibonde, baada ya leo Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaa Kamishna Suleiman Kova kumjia Juu
mtangazaji huyo na kumwambia aache utoto na kama anataka umaarufu atafute njia
nyengine.
Kauli hiyo Kamishna Kova imekuja siku chache baada ya Mtangazaji huyo wa
Kipindi cha Jahazi kujitokeza na kusema katika Vurugu zilizotokea mwishoni mwa
wiki iliyopita zilizofanywa na Vijana wa Panya Road katika maeneo mbalimbali ya
jiji hili,katika watu walikumbana adhia hiyo mtangazaji huyo alipata
matatizo,baada ya kudai kupigwa na vijana hao.
Kalipio hilo
la Kamishna kova ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na
Waandishi Habari alipokuwa akilizungumzia sakata la Panya Road,ambapo pamoja na
mambo mengine huku akizungumza pasipo kumtaja jina lakini tayari waandishi wa
habari walikuwa wamegundua anamlenga mtangazaji huyo,alisema inasikitisha watu
wanakuwa wanapotosha umma kiasi ambacho wangetakiwa kuwa wakweli kutokana na
kazi wanazofanya za kutoa habari kwa jamii.
“Hivi mtu
mwenye kama Yule tena maarufu sana na jamii inapenda kumsikiliza kwenye kipindi
chake kupotosha watu kwamba panya road wamemvamia inashangaza sana,maana jeshi
la polisi tumechunguza tumebaini akufanyiwa kitendo chochote kabisa, bali yeye
anafanya hivyo huku akitaka umaarufu wakijinga”alisema Kamishna Kova.
Kamishna kova aliongeza kuwa jamii
inahitaji watu kama hao kutoa taarifa za ukweli ila inasikitisha kuona wanataka
umaarufu wa kijinga ambao hauna tija katika jamii kwani umaarufu aliokuwa nao
unatosha kama mtangazaji huyo anataka kujilikana zaidi atafute njia nyengine.
Katika Hatua Nyingine Kamishna Kova aliwataja Viongozi wa watatu aliowakamata ambao walihusika katika
kusimamia vitendo hivyo vya kiovu ambao ni Halfani Nurdini miaka 24,mkazu wa
tandale Sokoni Jijini Dar es Salaam,Said Mohamed miaka 22 naye pia ni makazi wa
Tandale,
Viongoz wa Kundi hilo ni hawa hapa |
Mwengine ni
Mohamed Nangula Miaka 19 mkazi wa Mburahati kwa Jongo jijini Dar es Salaam
Hakuna maoni
Chapisha Maoni