LOWASSA NA MKEWE REGINNA WATOKWA MACHOZI,TIZAMA PICHA HIZI KUJUA
Waziri mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa mkono wa pole kwa waombolezaji katika Msiba wa aliekuwa muasisi na kiongozi wa kwanza wa Chama Cha TAA na baadaye TANU wilayani Monduli,Marehemu Mzee Lazaro Ole Ngoilenya Laizer aliyefariki juzi na kuzikwa leo Alhamis kijijini kwake Ngarash Monduli.Marehemu Mzee Lazaro Ole Ngoilenya Laizer ambaye ndiye alikuwa chachu kwa Mh. Lowassa na wanasiasa wengine wa Monduli kuingia katika siasa,amefariki akiwa na umri wa miaka 120,alioa wake 9 na kufanikiwa kupata watoto 53.
Waziri mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa mkono wa pole kwa wajane wa Marehemu.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mzee Lazaro ole Ngoilenya Laizer aliyefariki juzi na kuzikwa leo Alhamis kijijini kwake Ngarash Monduli
Hakuna maoni
Chapisha Maoni