BREEKING NEWS,WAZIRI MUHONGO AJIUZULU RASMI,ATOA MASHITI MACHAFU SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Aliyekuwa Waziri wa Nisharti na Madini Sospeter Muhongo Picha na maktaba
HABARI
zilizotufikia mda huu zinasema Hatimaye Waziri wa Nisharti na Madini Profesa Sospeter
Muhongo amejiuzulu katika nafasi
aliyokuwa nao .
Kwa mujibu wa Mwandishi wa Mtandao huu
KAROLI VINSENT aliyekuwepo Makao Makuu
ya Wizaya ya Nisharti na Madini iliyoko posta jijini Dar es Salaam ambapo ndio
kuna mkutano na waandishi wa Habari uliohitishwa mahususi kuzungumzia Hatima
yake. anasema Profesa Huyo msomi wa masuala ya Miamba nchini Ameamua Kuachia
ngazi nafasi yake akidai anawaachia wengine kwenye Nafasi hiyo kutokana na watu waameacha kuzungumzia masuala ya
maendeleo wanazungumzia mambo ya Escrow huku yeye hahusiki.
Profesa muhongo aliongeza kuwa hata mkataba wa Escrow ambao ndio umeleta yote
hayo anasema yeye hakuwepo wakati mkataba huo unasahiniwa.
“Mimi nashangaa leo watu kila kona naona
mimi ni mwizi, yaani kama mimi ndio nimechukua mabilioni ya escrow wakati
ukweli hupo wazi wakati wizara ya nisharti inaingia mwenye mkataba huo mimi
sikuwepo kwenye nafasi ya uwaziri,lakini leo watu bado wananiona mimi ni mwizi”
“Acha niaachia ngazi nafasi hii ya
uwaziri kwani imekuwa ni shida sana, mimi ni mtu msomi nimepata tuzo sehemu mbalimbali
duniani nasifika kwa kutoa ushahuri wenye tija,lakini leo naonekana
mwizi,wakati kiihistoria yangu mimi ni mtu msafi sina doa na wala sijawai hata
kumwibia mtu,lakini watu wananiona mimi mwizi”alisema Profesa Muhongo.
Aidha,Profesa Muhongo alisema kabla hajafikia
hatua ya kutangaza kujiuzulu aliwasiliana
na Rais Jakaya Kikwete alimuleze hatua nayotaka kuchukua ya kujiuzulu na
Rais akakubali kujiuzulu kwake.
Vilevile Profesa Muhongo aliendelea
kukanusha kile kilichotajwa na Ripoti ya PAC iliyomtuhumu kwamba yeye alikuwa
Dalali kati ya anayejiita na kuitwa mmiliki wa IPTL ambayo sasa ni PAP Bwana
Seith na Mkurugenzi wa VIP Engineering Bwana James Rugimalira na kusema
Kamati hiyo
imemuonea.
Kujiuzulu
huku kwa Profesa Muhongo kunatokana na mashinikizo mbalimbali kutoka ndani ya
nchi hususani Bunge pamoja na nchi wahisani ambao waligoma kutoa fedha za
Bajeti wakitaka wakiohusika na ufisadi wa Bilioni 320 kwenye Akaunti ya Tegeta
escrow iliyokuwa benki kuu BOT wachukuliwe hatua.
ENDELEA
KUFUATILIA MTANDAO HUU ULIoSHEHUENI WAANDISHI WALIOBOBEA KATIKA MASUALA YA
HABARI UTAPA TAARIFA KAMILI
Hakuna maoni
Chapisha Maoni