Zinazobamba

RAIS KIKWETE AFUMUA BARAZA LA MAWAZILI,DOKTA SLAA ASEMA HALINA JIPYA LIMEJAA WEZI TUPU SOMA HAPA KUJUA

http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/07/Jakaya-Kikwete1.jpg
pichani ni Rais Jakaya kikwete picha na Maktaba

NA KAROLI VINSENT
MDA mchache kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kulifumua baraza lake la Mawaziri na kuteua baraza jipya ambalo kufumuliwa kwake  kumetokana na Ufisadi wa zaidi ya Bilioni 320 kwenye Akaunti ya Escrow iliyokuwa kwenye Benki Kuu BOT.
    Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa ameibuka na kusema baraza hilo halina jipya lina lengo la kuwanufaisha marafiki zake walioko kwenye cha Mapinduzi CCM.
       Dokta Slaa ameitoa kauli hiyo mda huu wakati akizungumza na Mwandishi wa mtandao huu ambaye alitaka kujua baraza hilo jipya kwa upande wao wanalizungumziaje pamoja na mambo mengine alisema Rais kikwete anataka kulizima sakata la ufisadi wa Escrow katika kuwachagua watu ambao hawana jipya.
“Baada ya kuaona mambo yameaanza kumwendea hovyo kwenye chama chake ameanza kulivunja baraza la mawaziri mimi naona baraza hilo halina jipya limejaa watu wezi wenye nia ya kuendelea kuliibia taifa na watanzania wasitegemee makubwa”
“Kwani ufasadi wa Escrow umemgusa hata yeye mwenywe kikwete kutokana na mfanyakazi wake aliyemtuma kuchukua pesa kwenye Akaunti iliyofunguliwa kwenye benki ya Exim  kwa kumtuma bwana Guromu kuchukua pesa,leo anakimbilia kulivunja baraza la mawaziri hiyo haina jipya” alisema Dokta Slaa.
Baraza hilo aliloliteua hili hapa
Mabadiliko ya Mawaziri
.Mawaziri wawili wamejiuzulu
i) Ardhi-Tibaijuka
ii)Nishati na madini-Sospeter Muhongo
Walio teuliwa
1. George Simbachawene- Waziri Nishati
2.Mary Nagu-Waziri wa Nchi mawasiliano na Uratibu
3.Christopher Chiza-Waziri uwezeshaji na Uwekezaji
4.Halson Mwakyembe-Ushirikiano wa afrika mashariki
5.Lukuvi-Ardhi Nyumba na Makazi
6.Steven Wasira-Kilimo chakula na Ushirika
7.Samwel Sitta -Wizara ya Uchukuzi
8.Jenista Muhagama-Sera na uratibu wa Bunge


Hakuna maoni