ZIMWI LA UFISADI WA EPA LAMTESA CAG UTOUH,AWACHANACHANA WABUNGE SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni aliyekuwa mkaguzi mkuu na Mdhibiti wa hesabu za Ludovick Utoh akizungumza na waandishi wa Habari |
NA KAROLI VINSENT
ALIYEKUWA mkaguzi
mkuu na Mdhibiti wa hesabu za Serikali, Ludovick Utouh (CAG)ametoboa siri
alipokuwa katika nafasi hiyo na kusema katika maishani mwake hawezi kusahau
Ufisadi uliofanya kwenye Akaunti ya madeni ya nje ya EPA iliyokuwa Benki Kuu (BOT)
kutokana na Ufisadi huo kuwa tishio katika nchi na ulimfanya afanye kazi
katika presha ya Ajabu.
Pia akasema Ufisadi huo wa EPA ndio ulioibua neno Ufisadi
nchini.
Ludovick Utouh ameyasema hayo Mda huu
Jijini Dar Es Salaam mara baada ya kupokea tuzo ya heshima aliyotunukiwa na
Kampuni ya Dream Succes Enterprises kutokana na kutoa Mchango mkubwa na wenye
Tija katika Utawala wake katika Ofisi hiyo nyeti hapa nchini.ambapo pamoja na Mambo
mwengine bwana Utoh alisema -
katika
utawala wake licha ya kuibua mbambo
mengi ya ufisadi lakini ufisadi wa EPA
hatausahau kutokana ufisadi huo licha ya kuwa tishio katika nchi yetu ilimfanya
afanye kazi kwa presha sana.
CAG Utouh alisema baada ya kufanya kazi kwa presha sana ila
alifanikisha kuzipata nusu ya pesa ya Bilioni 66 kati ya bilioni 133 zilizoibiwa ambapo alisema ni tofauti na
nchi zengine.
Pichani ni Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali akipokea Tuzo huku hakiwa na Mkewe pamoja na Mtoto wake |
“Mataifa
mengi sana yanaibiwa,na serikali nchi nyingi zinazoibiwa pesa huwa hazifanikiwa kurudisha pesa zilizoibiwa ila
serikali yetu imefanikisha kurudisha pesa hizi zilizoibiwa kwahiyo ni jambo
jema sana”alisema Bwana Utoh.
Mbali
na Ufisadi wa EPA,Utoh alisema pia hawezi kulisahau sakata la aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nisharti na Madini,David Jailo baada ya kutuhumiwa na wabunge
kwamba amechangisha pesa kwenye taasisi zilizochini ya wizara ya Nisharti na
madini ili kuwahonga wabunge pesa iliwaipitisha Bajeti ya wizara hiyo-
Utoh
atabainisha kuwa pia sakata hilo lilimfanya
afanye kazi kwa Presha sana licha ya Mapendezekezo ya Kamati ya Bunge kutoa
mapendekezo ya yeye kuwajibishwa lakini amebaini wabunge wengi hawana uwezo wa
kusimamia Sheria.
“Sakata la jingiei
ni ripoti ya Jailo ambayo sito lisahau katika maisha yangu na hii ilitokana na
misimamo yangu kuwa tofauti na wabunge, na ikatuingiza kwenye mgongano ambapo
licha ya wabunge wale kutoa mapendekezo ya kuwajibishwa lakini kisheria iko
wazi kwamba wabunge wale hawana mamlaka ya kuniwajibisha”
Pichani ni Waandishi kutoka Vyombo Tofauti vya habari wakimsikiliza CAG |
“Na uchunguzi wangu ulibaini jumla ya milioni
140 zilizokusanywa na Bwana Jailo haikuwa kosa,na tulivyochunguza tukabaini
kwamba pesa zile zilitumika vizuri na hata hivyo kuchangishana pesa kwa
watendaji wa serikali sio kosa na hakuna kipengele cha sheria kinachomzuia
mtendaji wa serikali kukusanya michango na haya yote ni njia inaonyesha wazi
kwamba Wabunge wetu wanashindwa kuelewa
sheria”alisema Utoh
Kuhusu Ufisadi wa Akaunt ya Tegeta Escrow
Mkaguzi huyo
alisema kwa sasa hawezi kulizungumzia suala hilo kutokana na kuwepo kwenye
Mamlaka husika ila alisema Pesa
zilizotolewa kwenye Akaut ya tegeta Escrow ilikuwa ya ni ya Umma.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni