YAMETIMIA YANGA SASA,MRITHI WA JAJA APEWA RUNGU RASMI NI MBRAZIL EMERSON,SOMA HAPA KUJUA
Kiungo Mbrazil Emerson De Olivera Neves Roque pichani kushoto akisaini mkataba leo jijini Dar,wa kutumikia Klabu ya Young Africans,Kulia ni Afisa Habari wa klabu hiyo Baraka Kizuguto.
Dar es Salaam. Wakati Yanga ikimpa mkataba wa mwaka mmoja kiungo Emerson De Oliveira, watani zao Simba wamemtema rasmi mshambuliaji Paul Kiongera.
Emerson amesaini mkataba huo baada ya benchi la ufundi chini ya Mbrazil Marcio Maximo kuridhika na kiwango chake na sasa ataitumikia timu hiyo ya Jangwani.
Emerson aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" ambaye klabu hiyo imeamua kuachana naye baada ya kutoridhishwa na kiwango chake.
Ofisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa Maximo ameridhishwa na uwezo na kiungo mkabaji Emerson na kusema ataisaidia timu katika michuano mbali mbali ya Ligi na Kimataifa.
Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Yanga kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.
Katika hatua nyingine, klabu ya Simba imeachana rasmi na mshambuliaji Paul Kiongera anayesumbuliwa na majeruhi kwa muda mrefu na tayari mchezaji huyo ameshakubaliana na Simba kuhusu maamuzi hayo.
Habari za uhakika ambazo mtandao huu umezipata zinasema kuwa Kiongera huenda akaondoka nchini leo kwenda India kwa matibabu ya goti yanayomsumbua kwa muda mrefu.
Simba imelazimika kumuacha Kiongera baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na mshambuliaji Mganda, Danny Sserunkuma aliyekuwa akiichezea Gor Mahia ya Kenya.
"Ni kweli hatutakuwa na Kiongera, anatakiwa kupumzika baada ya matibabu. Hivyo lazima tuitumie nafasi yake," kilisema chanzo hicho.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni