YAMEFICHUKA-- IKULU YA KIKWETE YANUFAIKA MIPESA YA ESCROW,NI ZILE ZA BENKI YA STANBIC,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Rais Jakaya Kikwete picha na Maktaba |
MAJINA ya baadhi ya watu walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow zilizowekwa katika akaunti ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam yameanza kutajwa,Chanzo changu kinafahamu.
Miongoni mwa majina ambayo vyanzo vyetu vimethibitisha
kwamba yapo ni lile la mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye anaelezwa
kuchukua kiasi cha dola za Marekani milioni tatu (Sh. bilioni tano).
“ Tayari tunalo jina la mwanamke mmoja
ambaye amefahamika kama mke wa mmoja wa watu wenye vyeo vikubwa Ikulu. Kwa
sababu bado mapema kukupa jina kamili, vumilia kidogo hadi kila kitu
kitakapokamilika,” kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili kinachoshiriki
kwenye uchunguzi wa suala la namna fedha za akaunti ya Escrow zilivyolipwa kwa
watu.
Chanzo chaetu linahifadhi jina la mwanamama
huyo pamoja na mumewe kwa sasa kwa vile kuwataja majina kunaweza kuingilia
upelelezi.
Wakati majina ya baadhi ya mawaziri,
wanasiasa, majaji na viongozi wa dini yakionekana kulipwa fedha za mgao kutoka
katika akaunti moja ya Benki ya Mkombozi, kumekuwa na kitendawili kuhusu ni
akina nani hasa walilipwa fedha zilizokuwapo katika Benki ya Stanbic.
Wafaidikaji wengine wa akaunti hiyo
ambao Chanzo chetu limefanikiwa kuwapata kwa sasa ni mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la Rajiv Bharat Bhesania, anayetajwa kuwa mojawapo wa wasaidizi muhimu
wa mmiliki wa kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Seth Singh.
Katika mojawapo ya miamala katika
akaunti ya Stanbic iliyofunguliwa na PAP ambayo inaonekana katika ripoti ya
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Bhesania anaonekana kuchukua kiasi
cha dola milioni moja (shilingi bilioni 1.6).
Mtu mwingine ambaye inaonyesha amefaidi
fedha za akaunti ya PAP ni Mwanasheria wa PAP, Joseph Makandege, ambaye kampuni
yake ya sheria ya Bulwark Associates imeonekana kupata malipo yakiwamo ya
zaidi ya shilingi milioni 500 kwa nyakati tofauti.
Chanzo chetu kimefanya mawasiliano na mmoja wa wafanyakazi
wa zamani wa IPTL aliyedai kwamba Rajiv pengine ndiye mtu anayefahamu vizuri
zaidi mienendo na biashara nyingi zaidi za Sethi na kama Serikali inataka
taarifa za mfanyabiashara huyo mtata; basi inapo pa kuanzia.
Ingawa PAC ilipendekeza Sethi akamatwe
na kuhojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali kama vile utakatishaji wa fedha,
kukwepa kulipa kodi na udanganyifu, Raia Mwema limeambiwa kuwa mmiliki huyo wa
PAP hayupo nchini kwa sasa.
“Kama Serikali inataka kupata chochote
kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu
kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia
huyu.
“Nafahamu si rahisi kusema kila kitu
lakini nafahamu kwamba kama vyombo vya ulinzi vitambana kisawasawa, anaweza
kutoa siri zote za Sethi na hatimaye Watanzania wakapata wanachokitaka,”
alisema mfanyakazi huyo wa IPTL.
Malipo hayo yote yalifanyika katika
kupitia katika akaunti namba 912 0000 12 52 94 ambayo ilifunguliwa tarehe
28 Novemba mwaka 2013 na kufungwa tarehe 14 Septemba 2014.
Ni
katika benki hii ndiko ambako muamala wenye thamani ya shilingi bilioni 73.5
ulifanyika siku ya Januari 23 mwaka huu; muamala ambao sasa ndio unachunguzwa
na vyombo vya ulinzi.
Ni katika siku hii ambapo ripoti za
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ile ya
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), zilieleza kwamba kuna watu
waliondoka katika ofisi za benki hiyo wakiwa na magunia yaliyojaa fedha.
“Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu
walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo,
sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa,” ilisema sehemu ya ripoti
iliyowasilishwa bungeni na PAC.
Muamala huo unachunguzwa vikali na
Takukuru pamoja na ule wa Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi jijini Dar es
Salaam ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.3 zinadaiwa pia kuchukuliwa kwa siku
moja.
Habari za mke wa mmoja wa maofisa wa
ngazi za juu wa Ikulu kuhusishwa na uchotaji wa fedha za Escrow inakuja katika
kipindi ambacho Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Mbowe, akidai bungeni kwamba ofisi hiyo ya juu nchini ina mkono katika
utolewaji wa fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania.
Wakati akizungumza bungeni, Mbowe ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni,
alimtaja Prosper Mbena ambaye ni Katibu wa Ofisi ya Rais (Ikulu), kuwa ndiye
aliyeandika barua ya kuruhusu fedha zilizokuwa zimehifadhiwa zitolewe katika
akaunti hiyo.
Habari hizi za Stanbic kuhusishwa na
fedha za Escrow zimesababisha benki hiyo kumpa uhamisho aliyekuwa Meneja wake,
Paul Omara, ambaye sasa anadaiwa kurejeshwa nchini Uganda.
Omara anaelezwa kuitumikia benki hiyo
kwa muda wa miaka zaidi ya 11 na Raia Mwema limeelezwa kwamba ofisa huyo tayari
amehojiwa na Takukuru kuhusu suala hilo kabla hajaondoka.
Mmoja wa maofisa wa Takukuru
aliyezungumza na Chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa jina kwa maelezo kwamba
uchunguzi unaendelea, alisema wamepata ushirikiano mzuri kutoka Stanbic na kuna
uwezekano kwamba “ watu watakula Krismasi wakati tayari Takukuru ikiwa
imemaliza kazi”.
Suala la fedha za Escrow lililiteka Taifa
wiki iliyopita na sasa wananchi wanasubiri kwa hamu hatua itakayochukuliwa na
serikali kuhusu vigogo wanaotajwa kusaidia kutokea kwa kashfa hii.
Chanzo ni Gazeti la Raia Mwema
Hakuna maoni
Chapisha Maoni