Zinazobamba

KULEKEA XMASS-SUMATRA YACHACHAMAA NA MADEREVA,SOMA HAPA KUJUA

Pichani ni  Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA)  Dk Oscar Kikoyo.
Picha na Maktba
Na Karoli Vinsent
 BARAZA  la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA Limewakumbusha wamiliki wa Mabasi yaendayo  Mikoani na Madereva  kufuata  Masharti ya Leseni zao kwa  kutotoza nauli kubwa katika kipindi hiki cha Sikuku za mwezi Desemba na endapo mtu akikiuka sheria basi Mamlaka hiyo haitosita kumfutia Leseni  ya Basi litakalokwenda kinyume.
         Hayo yamesemwa  Mda huu Jijini Dar Es Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA)  Dk Oscar Kikoyo Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo,
       Dk Kikoyo alisema kutokana na wingi wa abiria na mahitaji ya usafiri kuwa makubwa katika kipindi hiki cha sikuku na kupelekea mahitaji zaidi ya usafiri ,baadhi ya watoa huduma wamekuwa  wakichukulia kipindi hiki kama njia ya  kuvuna zaidi kutoka kwa watumiaji  kwa kuongeza nauli maradufu.
     Dk Kikoyo aliongeza kuwa Baraza hilo linatoa wito  kwa Wamiliki wote wa mabasi kuwahimiza wafanyakazi na mawakala wao wanaokata tiketi katika vituo mbalimbali nchini kuwa waaminifu kwa waajiri wao na wateja wao.
      Vilevile Dk Kikoyo alisema baraza hilo likatoa wito pia kwa watu wote hasa Abaria wanaotarajiwa kusafiri kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kufanya maandalizi ya safari zao mapema ili kuepuka matatizo ya kulanguliwa tiketi na kupewa risiti tiketi watakazokata.
        Aidha,Dk Kikoyo alisema kuwa endapo abiria yeyote ambaye atatozwa nauli zaidi na kukataliwa kufanya Bookings zao mapema  basi asisite kutoa taarifa kwenye Mamlaka husika kwa namba ya simu 022 2127410,0787787621,0800110019 au 0800110020  ili Dereva wa Basi hilo pamoja na Mmiliki wake wachukuliwe hatua.


Hakuna maoni