UFAFANUZI KUHUSU MAFURIKO YA GHAFLA JIJINI DARESALAAM, HUU HAPA
Siku moja kupita baada ya mvua ya masaa mawili kuwaumbua wakurugenzi katika jiji la Daresalaam, sasa wakuu wa idara wameibuka na kutaja sababu za jiji hilo kufurika maji yaliojaa kinyesi katikati ya mji huo,
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, mmoja wa wakuu wa idara ya uhandisi kutoka manispaa ya Ilala, Eng. Bwigane Jaffari ameibuka na kuelezea sakata hilo na kusema kwamba sababu kubwa ya jiji hilo kujaa maji machafu kwa mvua ndogo ni kutokanana na wakazi wa jiji hilo kuwa wachafau kupita kiasi,
Bwigane ameendelea kusema kuwa changamoto hiyo ya wakazi wa mji wa Karikakoo, imesababisha mitaro kujaa takataka nyingi ambazo kwa hakika kwa usafi ambao manispaa inafanya uchafu huo usingeweza kuwepo,
Akielezea sakata la Mvua ya jana, Bwigane amesema tatizo ambalo limejitokeza jana ni kwamba wakazi wamekuwa wakitupa takataka hovyo katika sehemu isiyo rasmi na hapo ndipo chanzo cha maji kuanza kuama kutokana na brokeges kuwepo katika matundu ya mifereji,
Alipobana zaidi na mwandishi wa mtandao huu kuuleza umma ni kwa nini hasa sakata hilo limekuwa likijirudia kila mara, hususani nyakati ambazo mvua zinanyesha, Mkuu huyo wa idara ya Uandisi Manispaa ya Ilala, amekili kuwa tataizo hilo limekuwa likijirudia na sababu kubwa ikiwa niuchafu wa wakazi wa eneo husika.
NDG mwandishi katika manispaa yetu tunachangamoto kubwa mbili nayo ni uchafu uriokithiri toka kwa wakazi,unaweza kufanya usafi kwa nguvu kubwa lakini watu wamekuwa wakichafua mazingira hayo ndani ya Dakika kadhaa tu, hataukiangalia mafuriko ya jana, utaona chanzo ni kuziba kwa mifereji yetu ambayo imesababishwa na kutupwa kwa takataka, Alisema Eng. Bwigane,
aidha Bwigane ameongeza kusema kuwa wizi wa mifuniko ya mifereji unaofanywa na wakazi wa mji huu nayo imekuwa sabu kubwa inayohujumu miundombinu ya manispaa, na kwamba wizi huo unasababisha mifereji kujazwa taka kwa haraka kitu ambacho mvua ndogo ikija inakuwa ni kero kwa wakazi wa jiji.
Aidha Eng Bwigane amewatoa hofu wakazi wa jiji hili la Darsalaam kwa kusema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa matatizo ya kuziba kwa mifereji linakuwa ni historia katika manispaa yake
Mvua zilizonyesha juzi jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini jana,
zilisababisha maafa na kizazaa kikubwa kwa wakazi huku miundombinu
mbalimbali hususan ya barabara katika mitaa mbalimbali ikifinikwa maji.
Jijini Dar es Salaam, mvua hizo zilianza saa 4:30 asubuhi na kunyesha kwa nguvu kwa takriban saa mbili, hali iliyosababisha barabara katika mitaa mbalimbali ikiwamo ya Posta na maeneo ya katikati ya jiji hilo kufurika maji na kufanya magari kupita kwa shida.
Uchunguzi uliofanywa na fullhabari katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ulibaini kuwa maeneo mengi katika ya Jiji na mabondeni, yalifurika maji na kusababisha magari mengi na pikipiki kupita kwa shida huku na waenda kwa miguu nao wakitembea kwa taabu.
Hali hiyo ilisababisha foleni kubwa za magari katika baadhi ya mitaa hasa katikati ya Jiji.
Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za vifo katika Jiji la Dar es Salaam kutokana na mvua hizo licha ya kuwapo kwa usumbufu mkubwa kwa wakazi wake.
Wakati hayo yakitokea jijini Dar es Salaam, mkoani Tabora watu wawili, mke na mume, wakazi wa kijiji cha Lughubu kata ya Itumba wilayani Igunga, wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 11:00 jioni wakiwa wamekaa barazani kwenye nyumba wanayoimiliki wanandoa hao, Ernest Makala (90) na mkewe Pelepetua Petro (80).
Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mmoja wa watoto wa marehemu, Anastazia Ernest, alisema wazazi wake walikuwa wamejipumzisha nyumbani kwao, lakini ghafla ukuta wa nyumba ulibomoka na kuwaangukia walipokuwa wamekaa.
“Ni kweli sisi watoto tumepata pigo kubwa kwani wazazi wetu wawili wamefariki dunia, mimi nilipigiwa simu na majirani wakiniambia wazazi wangu wamepondwa na ukuta wa nyumba. Nilipofika katika eneo la tukio, nilikuta baba amefariki dunia," alisema Anastazia huku akibubujikwa na machozi.
Mtendaji wa kijiji cha Lughubu, Hussein Mohamed, alisema yeye baada ya kufika eneo hilo, alikuta wananchi wakiwa tayari wametoa kifusi cha udongo wa nyumba iliyoanguka huku mume, Ernest Makala, akiwa tayari amekwisha kufariki dunia.
“Mimi nilikuta tayari mwanaume akiwa amefariki dunia na mkewe alikuwa mahututi," alisema mtendaji huyo wa kijiji.
Alifafanua kuwa kutokana na hali aliyokuwanayo Pelepetua, wananchi waliamua kumkimbiza katika Kituo kidogo cha Afya kilichopo kata ya Itumba kwa matibabu, lakini Mganga wa kituo hicho, Efulay Malima, aliwashauri wampeleke Hospitali ya Wilaya ya Igunga.
Hata hivyo, alisema walipofika hospitali, Pelepetua alifariki dunia kabla ya kupewa matibabu.
Kaimu Mtendaji wa Kata ya Itumba, Twalib Ngahoma, aliwataka wananchi wa kata hiyo kuwa makini kwa kipindi hiki cha mvua za masika kwa kuchukua tahadhari mapema ikiwamo kutokaa karibu na nyumba zenye nyufa ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na miti iliyopo karibu na nyumba zao.
Aidha, mtendaji huyo alisema mbali ya vifo hivyo, pia nyumba 25 ikiwamo ya marehemu hao, zilianguka kutokana na mvua hiyo iliyonyesha siku tatu mfululizo.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Sono Nyaga, alithibitisha kufariki dunia kwa watu hao na kuongeza kuwa vifo hivyo vilisababishwa na kuangukiwa na kuta za nyumba waliyokuwa wakiishi.
HALI YA HEWA WATOA TAHADHARI
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), ilisema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa ni za kawaida na zitaendelea kwa siku tatu mfululizo.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agness Kijazi, alisema mvua za msimu wa vuli zimechelewa kwani zilipaswa kuanza Oktoba hadi Desemba, mwaka huu.
Alisema mvua zilizoanza kunyesha jana jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini, zimechelewa kutokana na Pwani ya Somalia kuwa na ongezeko la joto na upepo usio na unyevu nyevu kuvuma kuelekea ukanda wa Tanzania, hivyo kuwa na joto badala ya mvua huku kukiwa na mkandamizo mdogo wa hewa kwa upande wa Msumbiji.
“Ni hali ya kawaida ndani ya msimu wa mvua kuwa na uwezekano wa mvua kubwa…mvua hii itaendelea kwa siku ya kesho (leo) na Desemba 31, mwaka huu, ikipungua au kuongezeka kwa kiwango tofauti,” alisema.
Aidha, aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuwa uwezekano wa mvua kuwa kubwa upo, na kwamba inaweza kuleta madhara.
Dk. Kijazi pia aliwataka wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari kuhusu utabiri wa hali ya hewa wa kila siku

Hakuna maoni
Chapisha Maoni