Zinazobamba

SHINDANO LA MISS TANZANIA LAFUNGIWA RASMI,LUNDENGA AULA WA CHUYA,SOMA HAPA KUJUA

Pichani ni Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk baada ya kutangazwa mshindi picha na Maktaba

NA KAROLI VINSENT
BARAZA la Sanaa Taifa (BASATA) limeifungia shindano la Urembo la Miss Tanzania kwa muda wa miaka miwili kuanzia 2015 hadi 2016 kutokana na Shindano hilo kwenda kinyume na taratibu za (BASATA) ikiwamo kufanya makosa ya kijinai.
         Uamuzi huo Umetangazwa Mapema leo na  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa BASATA Godfrey L.Mngereza wakati alipokuwa akizungumza na Mwandishi Mtandao huu Ofisini mwa Baraza hilo  jijini Dar Es Salaam  ambapo Bwana Mngereza alisema Baraza limefikia Uamuzi huo baada ya kubaini mchakato wa uendeshaji wa Shindano ulivyokwenda katika msimu huu wa  mwaka 2014 wa Shindano la Urembo la Miss Tanzania ulikuwa na kasoro nyingi ambazo zilizopeleka taharuki kubwa kwa wananchi.
“Kabla ya kuanza Shindano la Miss Tanzania mwaka 2014,Baraza la sanaa Taifa tuliawandikia Uongozi wa LINO international Agency ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania kuwakumbusha kufuata taratibu za uendeshaji wa mashindano ya Urembo,kulipia Gharama zake,Zawadi za Washindi na Usajili wa mawakala watakaotumika kuendesha mashindano haya lakini hawakufanya hivyo kama kanuni zinavyotaka”Alisema Mngereza.
          Bwana Mungereza aliongeza kuwa baada ya kumalizika kwa shindano mapema mwezi Oktoba walifanya Tasmini ya ndani uongozi wa LINO international Agency ambao ni waendeshaji wa shindano hilo,wakabaini makosa kadhaa-
      Ikiwemo Zawadi za washindi kutothibitishwa kwa wakati,kukiukwa kanuni za uendeshaji wa Shinandano pamoja na (BASATA)
         Aidha,bwana Mngereza alisema mchakato wa kulifungia shindano hilo umejikita katika hatua mbalimbali ikiwemo   kushindwa kulipia gharama za kibali cha uendeshaji wa shughili za sanaa mwaka huu,mawakala waliohusika katika shindano hilo hawakusajiliwa ambapo walikwenda kinyume za kanuni za kampuni ya LINO no.9 (a) kinachosema mawakala wasajiliwe na BASATA,
Mikataba ya washiriki haikuwasilishwa kwa wakati pamoja na hundi ya malipo ya kibali Tshs.2,00,000/ iliyopelekwa Basata ilikuwa ni feki,kwani sababu hizo ndio zikaifanya baraza hilo kufikia maamuzi hayo.

        Vilevile, Bwana Mngereza akatoa wito kwa Makampuni yanafanya shughuli za Urembo nchini kufuata kanuni na Taratibu zinazowekwa na BA SATA ili kuepuka usumbufu unaonitokeza na kusema baraza hilo hili halitosita kuchukua hatua.

Hakuna maoni