SERIKALI YAJIPANGA KISAYANSI SOMA HAPA
Na Lorietha Laurence - MAELEZO
Serikali imejidhatiti katika kuboresha huduma za mawasilano kwa Njia ya Mtandao (TEHAMA) ili kurahisisha utendaji wa shughuli mbalimbali za kiserikali.
Akiongea na wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema lengo la Serikali ni kuongeza ufanisi kwa watumishi na jamii kwa ujumla kujifunza na kuwasilisha mada mbalimbali kupitia mtandao.
Balozi Sefua amesema kuwa serikali na taasisi zake mbalimbali hazina budi kutumia wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao kufanya shughuli zake zote zinazotekelezeka kwa njia ya Videoconference na Mafunzo ya Masafa ili kupunguza gharama.
“Lengo kuu la Serikali ni kurahisisha mawasilino baina ya watumishi na jamii ili kupunguza usumbufu wa safari ndefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine na pia kuokoa muda, na urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bwana Charles Sekondo, amesema ofisi yake imekuwa ikitekeleza majukumu kwa ufanisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaojihusisha na mafunzo kwa njia ya mtandao ili kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia duniani katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiserikali.
“Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao imerahisisha sana mawasiliano baina ya serikali, wizara, idara , wakala wa Serikali, pamoja na Sekta binafsi katika kuboresha uweledi kiutendaji kupitia utawala bora, anuai za jamii, maswala ya afya na mazingira” alisema Sekondo.
Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea maeneo mbalimbali ya ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao ikiwemo Sehumu ya Huduma za Video Conference, Chumba cha Maabara za Kompyuta na kituo cha taarifa za maendeleo (TDCI).
Mtandao wa TaGLA unajukumu la kuwajengea uwezo watumishi wa wizara, idara na wakala wa serikali pamoja na sekta binafsi katika nyanja mbalimbali ikiwemo , mafunzo ya midahalo kwa njia ya video ya hapa nchini na nchi nyingine, midahalo kwa njia ya mtandao, mafunzo ya ana kwa ana na mafunzo kwa njia ya uongozi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kulia) akitoa neno la shukrani kwa watu wa Kenya baada ya mazungumzo kwa njia ya mtandao , alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha IFM Pro. Daniel Mjema, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bwana George Yembesi na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Bwana Charles Senkondo.
Wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TaGLa) wakifuatilia mazungunzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) akifurahia jambo baada ya kupata maelekezo namna mitambo ya mawasiliano inavyofanya kazi kutoka kwa Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua wa kwanza kushoto,na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA ,Bwana Charles Senkondo(katikati) leo jijini Dar es Salaam.
Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua wa kwanza kushoto, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia) ya namana mikutano inavyofanyika kwa kutumia mtandao katika chumba cha mikutano wakati wa Ziara yake leo jijini dare s Salaam , wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akitembele ofisi za Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa) katika ziara yake leo jijini Dare s Salaam, mbele ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Bwana Charles Senkondo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondo akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika kituo cha taarifa za maendeleo(TDIC) alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondo akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika kituo cha taarifa za maendeleo(TDIC) alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ( wa tatu kushoto) akiangalia namna majadiliano yanavyofanyika kwa mfumo wa kutumia mtandao katika ofisi za Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa) wakati wa ziara yake leo jijini Dare s Salaam, wa kwanza kushoto ni Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua na wa pili ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa kwanza kulia) akiangalia moja ya vitabu vinavyohifadhiwa katika kituo cha taarifa za maendeleo kilichopo katika ofisi za Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake katika ofisi hizo , kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Bwana Charles Senkondo na wengine ni wajumbe wa bodi ya TaGLA.
Picha na Lorietha Laurence- MAELAZO
Picha na Lorietha Laurence- MAELAZO
Hakuna maoni
Chapisha Maoni