Zinazobamba

LICHA YA KUSHUTUMIWA NA MAGAZETI KWAMBA UENDAJI KUWA CHINI,NYALANDU AZIDI KUFANYA KAZI YAKE SOMA



Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai kuwa Serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha  hazina ukweli wowote.

Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo.

Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.

Akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki, Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.

Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.

“Nami niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akijaribu kurusha mkuki alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akitoka nje ya nyumba ya kimasai alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akionja maji kutoka katika kisima kilichojengwa kwa ajili ya kutatua tatizo la maji katika katika eneo la Loliondo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Wamasai waliokusanyika kwa ajili ya kusikia tamko la serikali juu ya uvumi wa kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Wamasai wakichukua kumbukumbu muhimu katika mkutano wao na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa jamii ya kimasai mara baada ya kumaliza mkutano nao.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael Rong’oi akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (aliyekaa kwenye pikipiki).
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiagana na mzee wa kimasai mara baada ya kumaliza mkutano uliokuwa na lengo la kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa jamii ya Wamasai katika eneo hilo.

Hakuna maoni