IKULU YA KIKWETE YAWAONEA HAYA WEZI WA ESCROW,YASEMA UCHUNGUZI WA BUNGE HAUTOSHI SOMA HAPA KUJUA
Ikulu imesema pamoja na kuwa Rais Jakaya Kikwete amekwishapokea
maazimio ya Bunge kuhusu wanaotuhumiwa kuchota Sh306 bilioni katika Akaunti ya
Tegeta Escrow, hawezi kuwachukulia hatua mpaka hapo uchunguzi kuhusu suala hilo
utakapokamilika.
“Rais lazima aagize vyombo vya uchunguzi kufanya kazi yake na
baada ya hapo ndipo atapata mahali pa kuanzia. Watu wengi walitaka Rais Kikwete
achukue hatua baada ya kupewa maazimio ya Bunge. Jambo hilo haliwezekani,”
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema jana na kuongeza kuwa hatua
zitachukuliwa kwa watakaobainika kuwa na makosa ya kimaadili au jinai baada ya
uchunguzi.
Alisema uchunguzi kuhusu uchotwaji wa mabilioni hayo uliofanywa
na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pia utazingatiwa na Rais katika kutoa
uamuzi.
“Maazimio ya Bunge ni mazuri ila inatakiwa muda kwanza ili Rais
naye apate taarifa za uchunguzi zaidi. Maazimio hayo ni muhimu na si ya
kupuuzwa hata kidogo,” alisema.
Alisema vyombo vinavyofanya uchunguzi kuhusu suala hilo ni vile
ambavyo vilitajwa kufanya hivyo katika maazimio manane ya Bunge.
Bavicha wamtaka Kikwete achukue hatua
Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), limemtaka Rais Kikwete
kuacha kuhamisha wakuu wa mikoa na badala yake atoe uamuzi wa kuwashughulisha
watuhumiwa wote waliohusika na kashfa ya escrow.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Bavicha, Mwita Julius
alisema: “Wakati huu si mzuri wa kuanza kuhamisha wakuu wa mikoa kwa kuwa ni gharama,
ni muda wa kuwachukulia hatua wahusika wote waliotajwa bungeni wakihusika na
sakata la escrow.”
Alisema Rais anatakiwa kuwashughulikia wateule wake wote
waliotajwa bungeni kwani wananchi wanasubiri kuona mabadiliko hayo kwa haraka.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni