HUJUMA YA SUKARI NCHINI--WAZIRI CHIZA AIBUKA NA ATOBOA SIRI YA WENYE VIWANDA,SOMA HAPA KUJUA
Pichana ni Waziri wa Kilimo,Chakura na Ushirika Eng. Christopher Chiza, Mb akizungumza na waandishi wa Habari leo |
Na karoli Vinsent
SIKU chache
kupita baada ya Wamiliki wa Viwanda vya Sukari nchini kusema viwanda Vyao viko hatarini kufa kutokana na serikali Kuendelea kuagiza sukari ya nje ya
nchini na kupelekea Sukari ya ndani kukosa soko nakuvifanya Viwanda hivyo kupunguza
wafanyakazi .
Naye Waziri wa Kilimo,Chakura na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb Ameibuka na kusema Kamwe Serikali haitoacha kuagiza
Sukari nje nchi kutokana na Viwanda Vilivyopo nchini kukosa uwezo wa kuzalisha
Sukari za Matumizi ya Viwandani kwani Viwanda vya ndani vinauwezo wa kuzalisha sukari za majumbani
peke yake.
Pia Waziri Chiza Akasema Tatizo ambalo
Serikali linakumbana nalo ni Uingizaji wa Sukari Kinyemela kutoka nje ya nchini
ambao ndio limekuwa kikwazo katika Viwanda hivyo.
Waziri Chiza ameyasema hayo Leo Jijini
Dar es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,aliouitisha mahususi
kuzungumzia hali ya Sukari nchini,ambapo pamoja na Mambo mengine Waziri Chiza
alisema Wamikili wa Viwanda vya Sukari wanashindwa kusema Ukweli kwa Umma,kwani
sababu ya Sukari zao kujazana kwenye Maghala inatokana na Viwanda hivyo kuzalisha Sukari
zenye matumizi ya Majumbani na sio Viwandani.
“Tazito hili la kulundikana kwa sukari na kukosekana wateja wasizingizie Sukari
zinazotoka nje ya nchi,kwani tatizo la sukari limetokana na Viwanda vya sukari
vya ndani haiviwezi kuzalisha Sukari kwa ajiri ya matumizi ya Viwandani na
Viwanda vinavyoitaji Sukari vinalazimikia kuagiza Sukari nje ya nchini ,na
wasipofanya hivyo Viwanda haviwezi kuzarisha bidhaa,na ndio
inatufanya tuagize sukari nje nchi”alisem Waziri Chiza.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo Tofauti vya Habari wakumsikiliza Waziri Chiza kwa Umakini |
Waziri Chiza aliongeza kuwa
Kinachotakiwa kwenye Viwanda hivyo sio kulalamika kwenye vyombo vya Habari
kwani hoja ya Waziri kuzuia kuto Vibari kwa Waingizaji wa Sukari ni kuudanganya
Umma kwani Vibari hivyo vinatolewa na Bodi ya Sukari nchini na kushirikiana na
Taasisi mbalimbali na sio Waziri wa huyo.
Aidha,Waziri Chiza aliongeza kuwa kwa
sasa hali ya uingizaji wa Sukari kwa magendo imekuwa kubwa sana na ndio sababu
inayofanya hata Viwanda vya ndani kushindwa kushindana na Sukari hizo kwenye soko la nchini.
Pia Waziri Chiza akasema kwa
sasa anashirikiana na Mamlaka za Ulinzi wan chi kupambana na Waangizaji wa Sukari kimagendo
kuhakisha wanachukuliwa hatua.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni