HABARI KUBWA LEO-RAFU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA-WAZIRI GASIA ASEMA NENO SOMA
Pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Gasia akizungumza na Waandishi wa Habari leo Picha na Suleiman Magari |
Na Karoli
Vinsent
SERIKALI nchini imekili Uchaguzi uliomalizika jana wa Serikali za Mitaa ulikuwa na Dosari katika
baadhi ya Maeneo mbalimbali nchini na kusema itawachukulia Hatua kali za
Watendaji Halmashauri Mbalimbali waliopelekea kuwepo na Dosari hizo.
Pia Licha ya kuwa na Dosari lakini
Badao Serikali imesema uchaguzi huo umefanikiwa kwa asilimia 98,Tofautisha na
Miaka mingine.
Hayo
yemesemwa leo Jijini Dar Es Salaam na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi) Hawa Gasia wakati wa Mkutano na Waandishi ili
kuzungumzia uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ambapo pamoja na Mambo Mengine
Waziri Gasia alikili kuwepo na Dosari kwenye Vituo mbalimbali vya kupiga kura katika baadhi ya Kata,Vijiji,Mtaa au Vitongoji
Waziri Gasia alizitaja Dosari hizo
ambazo ni kukosekana na Ujio wa Vifaa
vya Kupigia Kura,Kasoro za karatasi za kupigia kura,wapiga kura majina yao
kutokuwepo katika vituo pamoja na kuwepo na udangachifu kutoka kwa wapiga kura.
Pichani ni Waandishi wa Habari kutoka Vyombo vya Habari Tofauti wakimsikiliza kwa makini Waziri Hawa Gasia |
Vilevele Waziri Gasia alisema Halmashauri
na Maeneo yenye Kasoro ambayo hayakufanya Uchaguzi,yatarudia uchaguzi huo ndani
ya Siku (7) kama kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinavyoelekeza.
Aidha,Waziri Gasia aliitaja Mikoa
ambayo Dosari zilijitokeza na kupelekea kuhailishwa kwa uchaguzi huo katika baadhi ya Kata, vitongoji
na Vijiji ni, Kilimanjaro , Manyara,Morogoro,Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Mwanza,Tabora,Tanga,Mara,Rukwa,Dar
Es Salaam,pmoja na Mkoa wa Pwani.
Waziri Gasia aliongeza kuwa kwa ujumla
Halmashauri ambazo hazinadosari ni 145 kati 162 zilizofanya uchaguzi ambapo
Halmashauri tatu kati ya hizo hazikufanya Uchaguzi kabisa kutokana na
kucheleweshwa kwa Vifaa.
Hatahivyo Waziri Gasia aliziagiza Halmashauri
hizo uchaguzi kufanya haraka ndani ya siku 7 na vilevile Wizara hiyo ya
TAMISEMI itawachukuli hatua kali za watendaji waliopelekea Dosari hizo.
“Tumeitaka Mikoa Iwasilishe Taarifa rasmi
na kamiilifu kuhusu Kilichojitokeza
katika Halmashauri hizo na Wizara itachambua taarifa hizo ili kubaini wote
waliosababisha kasoro wachukuliwe hatua stahiki ikiwemo kusimamisha kazi,kukatwa
mishahara,pamoja na kufukuzwa kazi”alisema Waziri Gasia.
Waziri Gasia aliongeza kuwa licha ya
uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali za Mitaa kuwepo na Changamoto mbalimbali
lakini serikali imefanikiwa uchaguzi huu kwa asilimia 98 tofautisha na miaka
mingine.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni