HABARI ILIYOTIKISA JIJI-RAIS KIKWETE ACHARUKA AWATIMUA KAZI WAKURUGENZI,WAZIRI GHASIA AGOMA KUJIUZULU,ALIVAA GAZETI LA TANZANIA DAIMA SOMA HAPA
Pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia akizungumza na waandishi wa habari |
NA KAROLI
VINSENT
WAKATI ikiwa
Viongozi Mbalimbali wa Vyama vya Kisiasa pamoja na Wananchi wakiwalahumu
Watendaji wa Serikali kwa kufanya makosa na kupelekea kuwepo na Dosari nyingi
kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa ulimalizika Mwishoni mwa wiki iliyopita.
Nayo Serikali imeibuka na kuwafukuza kazi
Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini na wengingine ikiwasimamisha kazi kutokana na uzembe waliofanya uliopelekea kuwepo na dosari nyingi
kwenye uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa.
Hayo yametangazwa leo Jijini Dar es
Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia wakati wa mkutano na waandishi
wa Habari ambapo aliwataja Wakurugenzi waliosimaishwa kazi kutokana na Udhembe huo ni Felix T.Mabula-kutoka Hamalshauri,,Fourtunatus
Fwema Halmashauri ya Mbulu,Bi Isabella D,Chilumba kutoka Halmashauri ya Ulanga,Bi Pendo Malabeja kutoka Kwimba pamoja
na Wiliam Z Shimwela kutoka Sumbawanga.
Waandishi Wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakimsikiliza Hawa Ghasia leo jijin Dar |
Waziri Ghasia aliwataja tena wakurugenzi
ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana
na kupelekea Dosari hizo ni Bwana
Benjamini A Mojoro ,Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji Mkuranga,Abdalla
Ngodu,mkurugenzi Mtendaji wa Hamalshauri ya Kaliua,Masalu Mayaya,mkurugenzi wa
Kasulu,Bibi Goody Pamba mkurugenzi Mtendaji wa
Serengeti,Julius A madiga kutoka
Sengerema na Simon CR Mayeye mkurugenzi Mtendaji wa Bunda.
Vilevile,Waziri Ghasia alisema
Serikali pia imewapa Onyo kali ikiwemo na kuwaweka chini ya Uangalizi na kama
ikibainika wana udhaifu Mwingine Serikali haitosita kuwachukulia hatua ambao ni
Mohamed
A.Maje kutoka Halmashauri ya Rombo,Hamis Yuna kutoka Halmashauri ya Busega
pamoja na Jovin A Jungu kutoka Halmashauri ya Muheza.
Hatahivyo,Waziri Ghasia aliwataja pia
Wakurugenzi waliopewa onyo tu ni Isaya Mngulumi kutoka Manispaa ya
Ilala,Melchizedeck Humbe kutoka Manispaa ya Hai pamoja na Wallace J Karia
kutoka Mvomero.
Ambapo waziri Ghasia alisema uamuzi
huo wa kuwafukuza watendaji hao umetokana
na ripoti alizopokea kuhusu masuala yaliyojitokeza katika uchaguzi huo wa
serikali za mtaa na na kwenda kinyume na
sharia ya Ibara ya 36 (1) (4) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977 na Rais ameridhia kuchukuliwa hatua
hizo, ambapo pia alisema ni dhahiri kuwa wakurugenzi wa Halmashauri hizo -
Wameonesha
Udhaifu mkubwa katika kutekeleza Jukumu la Usimamizi wa Uchaguzi ambalo ni moja
ya majukumu ya ukurugenzi.
Alizitaja Kasoro walizofanya Wakurugenzi
hao ni Kuchalewa kuandaa Vifaa vya
kupigia kura,kukosa umakini katika kuandaa Vifaa hasa karatasi za kupigia kura
na zengine kuwa na Makosa,Kuchelewa kupeleka -
Vifaa kwenye vituo vya kupigia kura,Uzembe
katika kutekeleza Majukumu yao pamoja na kutoa taarifa za kupotosha kuhusu
maandalizi wa uchaguzi kuwa yamekamilika.
Katika Hatua Nyingine Waziri Ghasia
aligoma kujiuzulu na kusema hatua alizochukua ni wazi kwa wale waliohusika na akalitaka Gazeti la
Tanzania Daima kuandika Habari za Ukweli
na kuacha kudanganya Umma.
“Kiukweli nimeshangaa sana na
Gazeti la Tanzania Daima la Jana kusema eti CCM imepoteza zaidi ya Asilimia 80
Mkoa wa Mtwala,jamani kusema ukweli mimi ni Mbunge kutoka huko ,Halmashauri
zote za Mtwala CCM imeongoza kwa kishindo kikubwa inakuwaje Mwandishi tena
uliosomea kuandika habari ya uongo kiasi hicho”
“Na hili sijui mwandishi wa Gazeti hili
alikuwa anamaanisha nini na kama huyo Mwandishi wa Gazeti hili angekuwa
mtendaji wangu ningemwajibisha kwa kupotosha Umma”alisema Waziri Ghasia
Hakuna maoni
Chapisha Maoni