Viongozi wa juu wa Serikali ya Wanafunzi Kutoka Chuo Kikuu Huria wakimasikiliza Mtoa Mada Mussa h Omari
Wito umetolewa kwa Wanafunzi wa Chuo
Kikuu huria nchni kuuchukulia Ugonjwa wa Ukimwi kama Janga ambalo linahaja ya kupigwa
vita kwani ugonjwa huo umetajwa kuwa ni kikwazo katika kufikia malengo ya wanafunzi
katika chuo hicho kikuu.
Rai hiyo imetolewa mda huu Jijini
Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu huria nchini kampus ya Temeke Dk Jakrini
Bundala wakati Akifungua Semina kwa
wanafunzi wa chuo hicho kuhusu maambukizi Mapya ya Ukimwi,ambapo Dk Bundala alisema licha ya
chuo hicho kuzarisha wasomi mbalimbali nchini na nje nchi pia wanawajibu wa kuijenga jamii isiyokuwa na
Maambukizo mpya ya Ukimwi ndio maana chuo hicho wameandaa semina hiyo kwa wanafunzi kila
mwaka.
Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa
Chuo Kikuu huria Kampus ya Temeke Mganwa Nzota aliushukuru uwongozi wa Chuo Kikuu
huria kwa kuandaa Semina ya kupiga Vita Maambukizi Mapya ya ukimwi kwani kufanya
hivyo itasaidia kuijenga Jamii ya wanafunzi hao kutokuwa na Maambukizi ya
Ukimwi.
|
Hakuna maoni
Chapisha Maoni