Zinazobamba

MAHAKAMA KUUNDA KITENGO CHA HABARI



Ukakasi uliopo kati ya mahakama na wadau wa habari katika kupata habari bila wasiwasi umepelekea JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman,kusema kuna haja ya kuanzisha kitengo cha habari ili kuwasaidia waandishi kupata taarifa sahihi.

Akizungumza na mtandao huu hivi karibuni  jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano uliowakutanisha majaji, mahakimu na wahariri wa vyombo vya habari ‘Judicial Media Forum’ wenye lengo la kujadili misingi bora ya upashanaji habari baina ya tasisi hizo jaji huyo amesema wamedhamilia kuhakikisha kuwa mazingira ya kupata habari yanboreshwa kwa kuweka kitengo cha habari..
Alisema kuwa, waandishi wanatakiwa kuandika ukweli unaotokea kuhusu kesi iliyotokea au inayoendelea kwa lengo la kuufahamisha umma ukweli.
"Kumekuwa na makosa ya mara kwa mara yanayojitokeza kuhusu waandishi kuandika habari za kupotosha jamii kuhusu kesi fulani, lakini kwa ushirikiano huu nina imani waandishi watapata taarifa zilizo sahihi," alisema.
Akizungumzia kuhusu wanahabari kupewa ruhusa ya kuingia na vitendea kazi ndani ya mahakama, Jaji Chande alisema kuwa, wataangalia uwezekano kubadili sheria na kuwaruhusu kutumia vitendea kazi ndani ya Mahakama wakati kesi ikiendelea.
Katika mkutano huo, walipendekeza kuwepo na chombo maalum kwa ajili ya kutoa taarifa sambamba na mafunzo kwa waandishi wanaoandika habari za mahakamani, kwani zitawasaidia kujua misingi na taratibu za Mahakama.
Naye Rais wa Baraza la Habari (MCT), Jaji mstaafu Thomas Mihayo, alisema kuwa ni hatua nzuri iliyofikiwa kwa tasisi hizo kushirikiana, kwani itasaidia waandishi kupata habari zilizo kamili kwa urahisi.
Pia, aliwataka wanahabari kuzingatia miiko na sheria za taaluma ya habari, kwani itasaidia wao kuheshimika na kutoleta mitafaruku katika jamii.

Hakuna maoni