Zinazobamba

ZUNGU AWA MBOGO, HARUFU YA RUSHWA CBE YAMSHTUA, AEMA WALIOHUSIKA KUKIONA

Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Azani Zungu akikagua vimbweta katika chuo cha biashara CBE mapema hii leo na kubaini madudu makubwa katika zabuni ya kujenga vimbeta hivyo, mbunge huyo amesema ujenzi wa vibweta hivyo hamjamlizisha kutokana na ukweli kuwa mpaka sasa vimeonyesha kujengwa chini ya kiwango.

Mbunge wa jimbo la Ilala amekasirishwa vibaya na ubadhirifu wa fedha za mfuko wa jimbo uliofanywa na watu wa halmashauri hiyo kwa kujenga vibweta visivyo na ubora uliotarajiwa, huku fedha nying zikiingia katika mifuko ya watu wachache ambao hawakupaswa kula
Akizungumza na mtandao huu baada ya ukaguzi wa dharula uliofanyika katika chuo hicho mapema hii leo, Zungu amesema hakufurahishwa hata kidogo na fedha za mfuko wa jimbo zilivyotumika katika chuo hicho cha CBE na kusema kuwa atahakikisha kuwa watu wotewaliohusika kuhujum fedha hizo za walala hoi watawajibika ipasavyo,
Zungu ameendelea kusema kuwa tayari Diwani alitaka kujenga vibweta hivyo tena kwa ubora wa aina yake akini watu wachache waligoma na mwisho wa siku walichokifanya ni madudu matupu kwa vibweta vilivyojengwa.
Sula hili kwa kweli sikubali, tulisema hapo awali kuwa fedha za mfuko wa jimbo ni za watanzania ambao wanalipa kodi sasa iweje watu wanatumia kwa kufoji, nasema hili lazima nilisimamie,
Watanzania wanaona kama hatufanyi kazi na hiyo ni kutokana na watu wachache kuturudisha nyuma, lakini nasema hili lazima wahusika wawajibike 
Fullabari ilishuhudia Vimbweta hivyo vikiwa na nyufa, kitu ambacho kinaonyesha wazi kuwa material yaliyotumika ni ya kiwango cha chini.

Aidha katika hatua nyingine, Mbunge huyo amewataka wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho kuacha maramoja tabia za kuwarubuni wanawake na badala yake waruhusu akili zao kujikita katika masomo,
Aidha meendelea kusema kuwa, wanafunzi hao pia wanatakiwa kuwa mabalozi wazuri kwa kuwataka watabnzania kuanza kuamka na kupanga uzazi wao wa mpango
Zungu





Hapa mbunge huyo akiaini kitabu cha wageni katika ofisi ya mkuu wa chuo cha biashara,

Mkuu wa shule ya biashara CBE Prof. Emanuel Mjema akifafanua jambo mbele ya Mbunge wa jimbo la Ilala mapema hii leo, Mkuu huyo amesema chuo chake kinakabiliwa na matatiz makubwa a mindo mbinu ambayo hadi sasa limekuwa ni kero kubwa kwa wanafunz wanaosoma katika chuo hicho, miundombinu iliyopo iaruhusu wanafunzi wachache kupata huduma



Hapa akiwa amemaliza ziara yake ya kushtukiza katika chuo hicho cha CBE, Zungu amewataka chuo hicho kumpa orodha ya matatizo yao ili aone namna ya kusaidia kupitia kwa wadau mbalimbali na serikali kuu

Sehemu ya wanafunzi wakimsikiliza mbunge wao Zungu, wanafunzi hawa wamefurahishwa na jitihada anazoonyesha mbunge huyu kipenzi cha watu


Makam wa rais wa chuo cha biashara CBE kulia akifafanua jambo mbele ya mBunge wa Ilala, kushoto ni spika wa bunge la chuo cha CBE,uongozi huo wa chuo ulitumia fursa hiyo kuumuomba mbunge huyo awape fursa ya kutembeea bunge ambapo Mbunge huyo alikubali bila kipingamizi kuwapeleka jumla ya wabunge 65 ila kwa awamu





Hakuna maoni