MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI AWASHUKIA WATENDAJI,ASEMA WAACHE KUTUMIA MAABARA KUFANYA UCHAKACHUAJI,
Na Karoli
Vinsent
MSTAHIKI
meya wa Manispaa ya kinondoni Yusuph Mwenda amewataka Viongozi wamanispaa hiyo
kuacha kutumia nafasi ya kuwachangisha
wananchi kwenye ujenzi wa Maabara katika
shure za kata kama njia ya kufanya ufisadi badara yake wameaswa kuwa wazarendo.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es
Salaam katika kikao na madiwani wa Manispaa ya Kinondoni ili kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo
katika manispaa hiyo ambapo Mwenda amesema nia ya serikali ya kuwataka wananchi
kuchangia katika ujenzi wa maabara ni nia nzuri yenye kukuza sekta ya elimu
nchini na kuongeza wataalamu wa sayansi.
“kuhusu hili
la kuchangia maabara madiwani wengi wamelalamika kwamba kunawatu wanatumia
fursa hiyo kufanya ufisadi,kikweli siwezi kukataa kama tabia hiyo ipo,ila
nawataka vitendaji wa manispaa hii ya kinondoni kutumia fursa hii kama njia ya
kupata maabara nyingi na tuache kutumia fursa hii katika kufanya ufisadi kwani
hata viongozi wetu wa serikali nia ya kufanya hivi ni kuongeza wataaramu nchini
wa masuala ya sayansi”alisema Mwenda
Kwa upande wake diwani wa kata ya
mwabebande,Clement Boko CCM aliitaka Manispaa ya kinondoni kuweka ulinzi katika
kata yake ya Mwabepande ili kuiondoa hofu jamii ya maeneo hayo ambapo wamekuwa
wakiishi katika hali ya hofu kutokana na maeneo hayo kushamili vitendo vya
kihalifu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni