HABARI NZITO LEO--SAKATA LA KUPIGWA JAJI WARIOBA MAKONDA AIBUKA ASEMA UKWELI WA MAMBO SOMA HAPA KUJUA NI YAPI
Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita Baada ya aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Paul Makonda kumrushia Chupa aliyekuwa
Mwenyekiti wa tume ya ukusanyaji Maoni ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakati wa mdahalo wa
kutoa elimu kuhusu Katiba iliyopendekezwa na bunge Maalum la Katiba
, Mjumbe huyo ameibuka na kusema taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari,
kuhisika na vurugu kwenye Kongamano la kutoa
elimu ya katiba inayopendekezwa zilikuwa
na lengo la uchonganishi.
Na pia , amekanusha kumpiga jaji Warioba, huku
akisema waliofanya vurugu hizo jana, katika Ukumbi wa Mikutano wa Blue Peal, ni
kundi la watu lisilofahamu demokrasia na lina nia ya kuchafua taswira ya nchi.
Makonda akizungumza kwa uchungu alisema wakati
baadhi ya vijana wakianza kurusha viti alilazimika kumtoa katika ukumbi
aliyekuwa mjumbe mwenzake wa bunge hilo, Amon mpanju ambaye ni mlemavu wa macho
ili hasizurike na fujo hizo.
Hayo yamesemwa Makonda leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na waaandishi
wa Habari , ambapo alisema wakati akimtoa, Mpanju alifuatwa na Jaji Warioba akiwa na Prof. Paramagamba Kabudi, kujaribu kutuliza
vurugu hizo lakini hawakuweza kufanikiwa.
Makonda ambaye pia ni Kiongozi wa uhamisishaji
kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi CCM
alisema Baada ya hali kuwa mbaya ukumbini hapo, Jaji warioba alimtaka
kuhakikisha anamfikisha, Mpanju mahali salama huku wakijaribu kurudisha hali ya usalama ukumbini hapo.
Aliongeza
kuwa, wakiwa wanaondoka kupitia nyuma ya jukwaa alifuatwa naaliyekuwa mtangazaji wa radio ya Clauds Fm ambaye sasa ni mwandishi wa
Shirika la Utangazaji la Uingereza, Anord
Kayanda, akiwa amejeruhiwa kichwani akimtaka kumsaidia.
Makonda
alisema, ghafra kundi la watu lilimvamia na kuanza kumshambulia hali
iliyomfanya kuwaita walinzi kumwondoa jaji Warioba pamoja na Mapanju.
“Nilisika sauti za watu wakisema tumpige Makonda,
huyu ndiye aliyeandika katiba yenyewe, hivyo nilimsihi Mzee Warioba akimbie”
alisisitiza Makonda.
Kutokana na kundi hilo kuzidi kumshambulia, Makonda
alisema aliamua kukimbia hadi vyombo vya usalama vilivyofika kutoa msaada.
Alisisitiza kuwa , yeye alifika kwenye mkutano huo
kama mwananchi wa kawaida kusikiliza kile kilichokuwa kikijadiliwaa.
Akizungumzia
tuhuma za kuongoza vijana waliokuwa wamebeba mabango kwenye mdahalo huo,
alisema hakuwa akiwasiliana na mtu yeyote akiwa ndani ya mdahalo huo.
Alisema kama angekuwa anawaongoza vijana hao,
asingeweza kupigwa hivyo shutuma hizo hazina ukweli wowote.
Katika kongamano hilo lililoandaliwa na taasisi ya
Mwalimu Nyerere,
polisi walilazimika kuingila kati kumnusuru Jaji Warioba na
kulivunja kutokana na kuchafuka kwa hali ya usalama.
Kwa upande wake Msomi na mchambuzi wa Masuala ya
Kisiasa kutoka chuo Kikuu cha Dodoma Seiph Yahaya alisema Makonda hana cha
kujitetea kwa watanzania kwa kitendo chake hakikubaliki na mtu yeyote na
akakitaka chama cha Mapinduzi CCM kimvua uongozi Makonda kwa kitendo cha utovu
wa nizamu aliyofanya kwani chama cha mapinduzi kinasifika barani afrika kuwa na
viongozi wenye tija huku ikizingatia chama hicho kimsaidia nchi nyingi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni