Zinazobamba

AMKA ASUBUHI NA HABARI NJEMA KUTOKA MANISPAA YA ILALA,SOMA HAPA KUJUA

Pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Issaya Mussa akizungumza na waandishi wa Habari Jijin Dar Es Salaam picha na Seleiman Magari
Na Karoli Vinsent
KATIKA jitihada ya kupambana na Tatizo la Msongamano wa Magari katika Jiji la Dar Es Salaam,Manispaa ya Ilala na Temeke kwa kushirikiana na Kampuni toka china imeanza ujenzi wa barabara ya kisasa ambayo itaanzia Uwanja wa Ndege Jijin Dar Es Salaam kupitia Banana,kitunda ,msongora hadi Chamanzi Wilaya ya Temeke.
        Hayo yamesemwa Jana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Issa Mussa wakati wa Mkutano na Waaandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam,ambapo alisema Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.8 ambayo itakuwa na njia sita itawasaidia wakazi wa Dar es Salaam katika kupunguza Tatizo sugu la msongamano wa Magari.
      “Barabara hii itawasaidia sana wakazi wa Wiliya hizi mbili ambazo barabara hii inapita ambazo wilaya yangu ninayoinongoza ya Ilala pamoja na Temeke,kwani kumekuwa na Tatizo kubwa sana kwa wakazi wa Wilaya ya Temeke kutoka Chamanzi kuja uwanja wa Ndege ambapo awali iliwalazimu kupitia njia ndefu na kukaa sana kwenye barabarani lakini kwa ujenzi huu wa barabara wa Njia sita ukikamilika utaweza kuwaondolea Adha wakazi wa Wilaya hizi mbili”alisema Mussa.
        Mussa alizidi kusema kuwa mradi huo wa barabara umeanza rasmi mwezi wa nne mwaka huu kwa hatua za mwanzo za kufanyia tasmini ikiwemo maripo ya Fidia kwa wakazi ambao barabara hiyo itapita na kusema mradi utagarimu pesa za kimarekani Bilioni biloni 64 na pesa hizo zote ni kwa msaada wa Kampuni toka china na utarajia kukamilika mwezi 10,2016.
      “Kumbukeni barabara hii inajengwa kwa msaada wa Kampuni toka china ambayo ndio itakayosimamia ujenzi wote wa barabara hii na wao waneiomba serikali iwaondolee kodi tu wakati wa kuleta Vifaa vyao ambavyo vitatumika katika ujenzi wa mradi huu na Barabara hii imepewa Jina la “Kikwete Frendship Highway”alisema mkurugenzi Mussa.
        Vilevile Mussa alizidi kusema mradi wa barabara utakapoishia maeneo ya Chamanzi kutajengwa “Busneess Park”kubwa yakiwemo maduka makubwa ya Biashara ambayo yatamilikiwa na Kampuni ambayo imesaidia kujenga barabara hiyo na kuongeza kuwa maduka hayo yatasaidia kuwainua kipato wakazi wa Chamanzi na sehemu zengine.
      Aidha Mkurugenzi huyo akawataka wananchi kuupokea mradi huo kwa furaha kubwa na kuwa tayari kushirikiana na maafisa  ambao watakuja kutasmini nyumba ambazo zitapitiwa na mradi huo ili wapewe Fidia

Hakuna maoni