Zinazobamba

HABARI ILIYOTIKISA JIJI:KUPIGWA KWA WARIOBA SASA WANAHARAKATI WAMTAJA JK KUHUSIKA WADAI KWA NINI ANATOA KAULI ZA KEJERI DHIDI YAKIPIGO HICHO

MKURUGENZI WA KITUO CHA HAKI NA BINADAM AKIFAANUA JAMBO BELE YA WAANDISHI WA HABARI, KIJO AMESEMA TUKI LA KUPIGWA KWA WARIOBA NI LA KUPANGWA TENA NA GENGE LA WATU WACHACHE AMBAO WANATAKIWA KUCHUKULIWA HATUA MARA MOJA ILI HAKI ITENDEKE, AMESEMA KAMAVYOMBO HUSIKA HAVITACHUKUA HATUA BASI KAMA USHAHIDI UTAPATIKNA PRIVATE CASE ITACHUKUA MKONDO WAKE ILI HAKI IFICHURIWE
WAANDISHI WA HABARI WAKIMSIKLIZA KIJO BISIMBA AKIFAFANUA MAMBO MBALIMBALI KATIKA MKUTANO WAKE NA ASASI ZINGINE ZIPAZO SITA MAPEMA HII LEO.
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA SIKIKA TANZANIA AKIFAFANUA JAMBO MBELE WA WANAHABARI, MKURUGENZI HUFO ALISEMARAIS AMEMKELI WARIOBA KWA KAULI YAKE YA KUOMBA YASIMKUTE KAMA YALE YA WARIOBA,NI KAMA AMEUNGA MKONO KIPIGO CHAKE
NKYA AKIFAFANUA KATIKA MKUTANO HUO
Kufuatia kupigwa kwa waziri mkuu mstaafu Jaji joseph Sinde Warioba, sasa Asais mbalimbali zimeanza kujitokeza kutoka kila kona na kuanza kulaani kitendo hicho kwa kusema kwamba ni kitendo ambacho kimelenga kuwatisha watanzanaia wenye nia ya kujadili katiba pendekezwa wasiijadili kwa uwazi na uhuru,

Wakizungumza na waandihsi wa habari mapema hii leo, asasi mbalimbali za kiraia  ambazo zimeungana na kutoa yao ya moyoni kuhusu hatua za kupigwa kwa jaji huyo mwenye heshima kubwa hapa nchini, wasema kuwa wameamua kutoa tamko lao baada ya kuona kuwa kupigwa huko kulikuwa na nia ovu dhidi ya mchakato mzima wa kujadili katiba pendekezwa,

Asasi hizo zilizoongozwa a kituo cha sheria na haki za binadam, pamoja na kile cha Jukwaa la katiba hapa nchni wamesema hatua ya kulaani imekuja kufuatia kuvunjiwa heshima kwa kiongozi ambaye ana heshima kubwa hapa nchini ambaye amejitoa kuhakikisha kuwa maslahi ya watanzania yanafiikiwa tena kwa uwazi,

Kufuatia kupigwa kwa kiongozi huyo, asasi hizo zimeitaka serikali kupitia vyombo vyake vya dola kuchukua hatua mara moja ili kuondoa sintofahamu ambayo mpaka sasa imeendelea kuwakumba wananchi wa Tanzania,

"Tunachojua ni kwama watanzania waliona ile vurugu na wahusika wanatambuliwa tunaomba basi watu hao wawez kuchukuliwa hatua mara moja, hivi ni kwanini mpaka sasa bado kuna kigugumizi katika kuchukua hatua kwa watu hao ambao ni wachache ,

Akisoma tamko la asasi za kiaraia kwa waandishi wa habari, Msomaji wa tamko hilo Bi Hellen Kijjo Bisimba Ameweka wazi kuwa tukio la kupigwa kwa warioba lilipangwa na genge la watu wachache ambao walikuwa na nia ovu ya kuharibu mkutano huo abao ulilenga kutoa elimu kwa wapiga kura,

Aidha asasi hizo ambazo zilikuwa zikiongea kwa uchungu kutokana na kupigwa kwa Warioba, Wameionya vyombo vya dola kuhakikisha kuwa huo unakuwa ni mara ya mwanzo na ya mwisho kutokea kwa vurugu kama hizo kwani kitendo cha kuachilia hali kamahiyo kuendelea kutokea kutalipelekea taifa katika vita dhito amabayo itagharimu maisha ya awatanzania wote,

WALAANI KAULI YA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO

Aidha katika hatua nyingine mkurugenzi wa shirika la Sikika Ndg Irinet Kirya amelaani kauli ya Rais ya jamuhuri ya muungano wa Tanznaia kuwa kauli hiyo ni ya kejeli na iliyolenga kujenga makundi miongoni mwa waanzanaia,

Kirya amesema kauli ya hivi karibuni ambayo aliitoa mkuu wa nchi akiwa huuko mwanza imezua maswali mengi huku wengine wakisema kuwa kauli hiyo imeunga mkono kwa asilimia mia moja kupigwa kwa mzee wetu Joseph Sinde Warioba, 

Rais Jakaya Kikwete alinukuliwa akisema  anaomba yasimkute ya Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba aliyeshambuliwa katika mdahalo wa katiba uliofanyika Dar es Salaam, juzi.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo huko  Mwanza  katika mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kupambana na Rushwa (Safac) unaojumuisha nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc).
Hii ndiyo kauli ya rais “Naamini Katiba Inayopendekezwa itapitishwa, nina matumaini hayo. Nadhani na mimi nitakavyokuwa napiga kampeni hayatatokea yale ya jana(juzi), maana mie sioni haya kuipigia kampeni kama wale wenzetu ambao wanataka isipite,” alisema Rais Kikwete kwa ufupi.
Juzi, Jaji Warioba alishambuliwa na kundi dogo la watu walioingia katika mdahalo ulioitishwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kutolewa chini ya ulinzi.
Vurugu hizo zilitokea wakati Jaji Warioba alipokuwa akihitimisha hotuba yake kwa kuhoji watu wanaotumia vibaya jina la Mwalimu Julius Nyerere kupitisha hoja zao katika misingi isiyokubalika.

Miongoni mwa wanaotuhumiwa kumshambulia Jaji Warioba ni Katibu wa Hamasa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM), Paul Makonda ambaye hata hivyo, jana alikana kufanya kitendo hicho.


Hakuna maoni