Zinazobamba

BREEKING NEWZZZZZZZZZZ: MKURUGENZI TPDC NA MWENYEKITI WAKE WATUPWA RUPANGO DAR, KISA NI UFISADI




Kaimu Mkurugenzi wa TPDC na mwenyekiti wake wa bodi watupwa rumande kufuatia kushindwa kuwasilisha mikataba 26 kwa PAC.

Taarifa zilizotufikia hivi punde ndani ya chumba cha habari, kinaleleza kuwa Kaimu Mkurugenzi wa TPDC,bwa.James Andilile na Mwenyekiti wake wa bodi bwa.Michael Mwanda wamepelekwa rumande kwa kosa la kutowasilisha mikataba 26 kwa kamati ya bunge la hesabu za mashirika ya umma PAC,Kamati imeagiza wapelekwe huko na hatua zichukuliwe dhidi yao
 

 Polisi Dar wamewakamata M/Kiti wa Bodi na Kaimu Mkurugenzi wake wa TPDC leo kwa kushindwa kuipatia Kamati ya Bunge (PAC) mikataba 26 ya gesi tangu 2012


Huyu ndiye anayedaiwa kuwekwa rumande na mwenyekiti wake kwa kosa la kushindwa kupeleka mikataba mbele ya kamati ya bunge

Awali KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imelipa siku mbili Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Petroli Tanzania (TPDC), kuhakikisha inakabidhi mikataba na taarifa ya mikataba ya gesi kwa Katibu wa Bunge. Agizo hilo lilitolewa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya TPDC kushindwa kutekeleza maagizo ya kamati hiyo iliyotoa takribani mwaka mmoja, hivyo kushindwa kuendelea kupitia hesabu za shirika hilo za mwaka 2012/13.

PAC iliitaka TPDC kuhakikisha inawasilisha mikataba yote 26 ya gesi, kuwasilisha taarifa ya mapitio ya mikataba ya gesi na kutoa taarifa ya ujenzi wa bomba la gesi, agizo pekee ambalo shirika hilo limelitekeleza.

“ Jumatano (kesho) kabla ya muda wa kazi kuisha muwe mmepeleka mikataba yote ya gesi na taarifa ya mapitio ya mikataba hiyo ili tuwapangie muda mwingine wa kupitia hesabu za taasisi yenu.”

Kabla ya kutoa maagizo hayo, Zitto pamoja na Makamu wake, Deo Filikunjombe walihoji bodi na menejimenti ya TPDC ni kwanini wameshindwa kutekeleza maagizo ambayo kamati hiyo ilitoa mwaka mmoja uliopita.

“ Kazi ya Bunge ni kusimamia Serikali, hivyo kamati hii ina uwezo wa kuhitaji taarifa yoyote isipokuwa inayohusu usalama wa nchi. Tukihitaji taarifa kwa IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi), Mkuu wa Majeshi na Usalama wa Taifa wanakuja hapa na kumuonesha Mwenyekiti ambaye anatoa taarifa kwa wajumbe.

“ Hata hii (akionesha taarifa ya NARCO) imeagizwa na Rais lakini kamati inayo, sasa kwanini ninyi mmeagizwa kuleta mikataba na taarifa ya mapitio ya mikataba mmeshindwa kufanya hivyo na mmefanya kwa sheria ipi?” alisema Zitto ambaye alionesha wazi kuchukizwa na hatua ya TPDC kutotekeleza maagizo hayo.

Alisema: “ Hii ni kamati ambayo imepewa madaraka ya kuhitaji nyaraka na taarifa yoyote kutoka kwa mtumishi wa serikali ;na pia ina uwezo wa kutoa adhabu kwa mtendaji yeyote wa serikali ambaye anakataa kutekeleza hilo”.



Alisema pamoja na kutoa siku hizo mbili kwa TPDC kuwasilisha mikataba na taarifa za mikataba ya gesi, Bunge limeahidi kuwapangia muda mwingine wa kupitia hesabu zao na mikataba saba iliyokaguliwa itenganishwe na ile 19 ambayo bado hajakaguliwa.

Akijibu hoja, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda alisema taarifa ya mapitio ya mikataba ya gesi, imepelekwa kwa Waziri wa Nishati na Madini, ambaye ndiye aliyeandika hadidu za rejea za kutaka kufanyika kwa mapitio hayo.

Aidha, kuhusu mikataba, Mwanda alisema kuwa mikataba hiyo iko ofisi za Bunge na kuwa kamati au mbunge anayetaka kuiona, anatakiwa kufuata taratibu za kuangalia mikataba hiyo.

Wakati huo huo, PAC imeiagiza ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali (CAG) kuhakikisha inafanya ukaguzi katika wizara zote kuhusiana na fedha zinazotumika kwa ajili kulipia matangazo ya hotuba za bajeti za wizara.

Maagizo ya PAC yalitolewa na Zitto alipokuwa amekutana na Wizara ya Nishati na Madini na kuwa ukaguzi huo utasaidia kujua kama njia inayotumika ni muafaka au kuja na njia ambayo ni nzuri na ambayo haitatumia fedha nyingi.

Aidha, Zitto alisema Wizara ya Nishati na Madini wakati wa kikao kichacho wizara hiyo ije na taarifa ya wamefikia wapi mchakato wa ziara hiyo kutumia risiti za kielektroniki katika kulipa na kulipwa fedha.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Eliakim Maswi alisema Sh bilioni 400.9 kati ya Sh bilioni 648 za maendeleo zilizopangiwa na wizara hiyo, zilitumiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wakati wa tatizo la umeme nchini.

Maelezo ya Maswi yanatokana na swali la Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Pwani, Zainabu Vulu aliyetaka kujua Sh bilioni 4465 zilizopelekwa Tanesco zilikwenda kutumika kwenye miradi gani.

CHANZO: Habari Leo

Maoni 1

Bila jina alisema ...

NAJIHURUMIA MIMI PAMOJA NA WATANZANIA WEZANGU WOTE MASKINI ZAID YANGU RASILIMALI ZA NCHI YETU ZINAWANUFAISHA WALIONACHO TU,
ZITTO UMEJITOLEA KWELI LAKINI HUNA WAKUKUSAIDIA AMBAYE HALENGI KUPATA MASLAHI BINAFSI