HABARI KUBWA ASUBUHI HII-SITTA ALIUA TAIFA,UBABE WAKE AKIWA SPIKA WATAJWA,SOMA HAPA KUJUA
Na Karoli
Vinsent
HATUA ya
Samwel Sitta akiwa spiaka wa Bunge la Jamhuri ,ya kuzima mjadala juu ya
mikataba ya serikali kufikishwa bungeni ,imegundulika kuwa ni kichaka ambacho
serikali kuendelea kujificha na kukataa
kufikisha mikataba hiyo Bungeni,MTANDAO HUU umebaini.
Azimio Na 13 la Bunge Juuu ya Mkataba tata
kati ya serikali ba Kampuni ya kufua Umeme wa dharula ya Richmonf Development
Company (RDC) ililitaka wazi serikali
iweke mikataba yote wazi bungeni ili kila mwananchi aione na kuweza kuondoa
mianya ya kifisadi.
Lakini wakati wa kijadili maazimio 23
yaliyojadiliwa na kamati Teule iliyoundwa kuchunguza mazingira ya udanganyifu
katika mkataba huo,Samwel Sitta alisimamia kidete na kutaka Mamlaka ya Juu kuhamua suala hilo.
Kitendo hiko
cha Sitta kufanya hivyo ndio kimefungua Mwanya kwa watendaji wengi wa serikali
kutumia fursa hiyo kuingia kwenye mikataba ya kifisadi kwa kisingizia cha usiri
.
Azimio
lilikuwa linapiga marufuku serikali kuendelea na kile kilichoitwa ni “Utaratibu
uliorithiwa kwa wakoloni na kujigeuza
kuwa mazoea wa kuzuia mikataba ya kibiashara kuwekwa wazi hata kwa walipa kodi
wenyewe.
Bunge lilitaka mikataba yote ya
Madini,Gesi,Mafuta,ununuzi wa mitambo na mingine ambayo watendaji wa serikali wanaingia kwa
niaba ya nchi ifikishwe bungeni ijadiliwe,ilidhiwe na kuidhinishwa.
Duru mbalimbali zinasema “kama sio sitta
kusitisha mjadala kabla ya bunge kuing’ang’aniza serikali leo kusingekuwa
kichaka cha kuficha mikataba yote ya serikali.
“Spika sitta alikatiza mijadala kuichia
mamlaka na mamlaka imekataa kuchukua hatua na hapo ndipo tulipofikia tunafichwa
mikataba”
Hadi Sitta anafunga mjadala huo wa
Richmond Bungeni agizo hili alikutekelezwa ,jambo ambalo limetoa mwanya
kwa kwa serikali kuendelea kufanya
mikataba kuwa ya siri.
Madai kuwa maamuzi ya Sitta kuhusu Richmond
yanaendelea kuliangamiza taifa ,yameibuka wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Mashirika ya Umma (PAC),ikikwaruzana na shirika la Petroli Tanzania (TPDC)
kuhusu Mikataba ya Gesi
Michael
Mande ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC,aligoma kuwasilisha mikataba hiyo
bungeni kwa madai “Sheria inakataza kuwasilisha mikataba ya aina hiyo bungeni
PAC
inaongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe
Mande
alisema “Hatuwezi kuleta taarifa zetu mbele ya kamati kwasababu sheria
haituruhusu kufanya hivyo”
Usiri huo wa
mikataba ndio umetajwa kuliingiza taifa katika ufisadi wa kutisha, na kiongozi
anayetajwa kulifikisha taifa huko ni Samwel Sitta kipindi alipokuwa Spika wa
Bunge ambaye alipuuzia Suala hilo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni