FREEMAN MBOWE ALIOKOA TAIFA,HICHI NDICHO ALICHOKISEMA JANA
Sintofahamu iliyotokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma Ijumaa Novemba 28, 2014 imepelekea Spika Anne Makinda kulazimika kusitisha shughuli za Bunge mpaka hapo watapojadiliana tena.
Hii ni baada ya majadiliano makali kuhusu kuwajibishwa ama la kwa viongozi wanaohusika na sakata la akaunti ya Escrow. Hali hii iliibuka baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA na kambi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe kuinuka na kusema kuwa Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, na kwamba kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kutoka maamuzi kwa mamlaka ambayo yako ndani yao.
"Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi", alisema Mhe. Mbowe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni