WIZI WA BILIONI MOJA STANBIC--JESHI LA POLISI LAFAFANUA HAYA..
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
24/10/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
POLISI KANDA MAALUM KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA
BENKI ILI KUBAINI NJAMA ZA WIZI
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukagua
kikundi cha Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kilichoundwa na Polisi
wakishirikiana na wananchi wa kata ya Keko Magurumbasi. Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Benki zote na
taasisi za kifedha kabla ya kuajiri wafanyakazi ni vizuri wafanyiwe upekuzi
yakinifu (Vetting) ikiwa ni pamoja
na kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwachukua alama za vidole(Finger Print) na kuchunguza katika
maabara ya Jeshi hilo(Forensic Bureau)
kama wafanyakazi au walinzi wamewahi kujiingiza katika makosa ya jinai kabla. Aidha hivi karibuni umezuka mtindo wa baadhi
ya wafanyakazi wachache wa benki kushiriki katika matukio ya wizi
ndani ya Benki, ikiwa pamoja na kupanga mikakati
ya kufanikisha wizi huo kwa kushirikiana
na wahalifu
Mnamo majira
ya saa nne na nusu Tarehe 23/10/2014 asubuhi, Stanbic Benki Tawi la Mayfair Plaza Mikocheni,
majambazi wapatao 10 mmoja akiwa na bastola walivamia na kuwaweka chini ya
ulinzi wafanyakazi na kufanikiwa kuiba mamilioni ya pesa, aidha katika
uchunguzi wa awali imebainika ni mpango wa ndani ya benki( Inside Job) ambao ulipangwa ili kukamilisha wizi huo. Jeshi
la Polisi linafanya msako mkali ili
kuwabaini wahusika hao ili sheria ichukue. Tanzania ni nchi ya amani hivyo haitakiwi kuharibiwa sifa zake wawekezaji au wananchi. Aidha kuanzia sasa Benki
zote zitalindwa kwa ushirikiano na kampuni za ulinzi zenye vifaa vya kisasa
ikiwa pamoja na silaha za moto.
JESHI LA POLISI LAKANUSHA VIKALI KUHUSU UVUMI WA
KUTEKA WATOTO JIJINI DAR ES SALAAM.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukagua kikundi cha
Polisi jamii na ulinzi shirikishi kilichoundwa na Polisi wakishirikiana na
wananchi wa kata ya keko magurumbasi
kamishna kova alikanusha vikali juu ya uvumi unaoendelea jijini Dar es
Salaam kuhusu utekaji nyara wa watoto wadogo wanaosoma shule. Hivi karibuni
umezuka uvumi kutoka kwa watu mbalimbali hasa wazazi ambao uvumi huu umewafikia
kwamba kuna kundi la wahalifu wanaotumia gari aina ya NOAH rangi nyeusi ambao
kazi yao ni kuteka nyara wanafunzi kwa nia ya kutenda uhalifu ikiwa ni pamoja
na kuwachuna ngozi na madhara mengine.
Mpaka
sasa Jeshi la Polisi halina taarifa yoyote ya mtoto kutekwa au kufanyiwa
madhara yoyote kwa mtindo wa utekaji nyara. Pia Jeshi la Polisi limegundua
kwamba huu ni uvumi ambao haujulikani chanzo chake hivyo wananchi wanaombwa
kuachana na uvumi huo na kuupuuza kwani unaleta hofu katika jamii bila sababu
za msingi.
Aidha, Jeshi la Polisi linapenda kuwatoa hofu
wananchi na pindi wakiona mtu yeyote anayeeneza habari hizo watoe taarifa kituo
chochote cha Polisi
S. H. KOVA
KAMISHNA WA
POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
Hakuna maoni
Chapisha Maoni