HABARI KUBWA LEO--TUME TAIFA YA UCHAGUZI YAMFUNGA MDOMO JAJI WEREMA YATANGAZA RASMI UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUPIGA KURA,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na Karoli
Vinsent
HATIMAYE
tume Taifa ya uchaguzi nchini imemaliza ubishi uliokuwepo kati ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tarehe ya
kufanyika kura ya maoni ili kupitisha Katiba iliyopendekezwa na bunge Maalum la
katiba ambapo mwanasheria huyo mkuu alisemwa kura ya maoni itafanyika mwezi wa tatu mwakani
na Rais Kikwete akasema mwezi wa nne mwakani ,
Baada ya leo tume hiyo kusema itaanza
kuwaandikisha wapiga kura wapya na wazamani kwaanzia mwezi Novemba mwaka huu nchi kwa nchi nzima na
kukamilisha zoezi hilo tarehe 18 mwezi wa
nne mwakani 2015 na kura ya maoni kufanyika mara moja.
Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar
es Salaam na Makamu mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini (NEC) Jaji
Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahamoud Hamidi wakati wa Mkutano na Waandishi wa
Habari,ambapo Jaji Hamid alisema baada
ya kupata Vifaa vya uboreshaji wa kutoka serikalini na kutoa mafunzo kwa watendaji wa tume hiyo
ili waweze kufanya kazi kwa usahii basi kwaanzia mwezi novemba mwaka huu
uboreshaji wa Daftrari la kupiga kura utaanza .
“Tume imepanga kufanya zoezi la majaribio ya uboreshaji wa
Daftrari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa Biomtetric Vote
Regislation katika majimbo matatu ambayo ni kawe jijini Dar es salaam na
kilombero pamoja na Mlele manispaa ya katavi, katika mwezi huo wa novemba na zoezi hilo
litaanzania kwaanzia saa2.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni katika vituo husika”alisema
Jaji hamid
Jaji Hamid
alisema baada ya kukamilika zoezi la majaribio la uboreshaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura kitakachofuata ni kuanza kwa uboreshaji katika maeneo
mengine ,na wanatarajiwa kufanya uboreshaji huo katika miko nchi nzima
isipokuwa na Mkoa Dar Es Salaam na Zanzibar ambao wao uboreshaji utanyika baada
mikoa yote itakapomalizika
Ambapo alisema uboeshaji huo utafanyika kuanzia
mwanzoni mwa mwezi Januari,2015 hadi katika ya mwenzi Februari,2015 katika
mikoa yote isipokuwa mikoa ya Dar es Salaam na Zanzibar,
“Uandikishaji wa mikoa ya Dar es
Salaam na Zanzibar utafanyika mwishoni mwa mwezi Februari,2015 na uandikishaji huu
katika mikoa yote utafanyika kwa awamu nne (4) katika kila halmashauri ili
kutoa fursa ya kuhamisha vifaa vya uandikishaji kutoka eno moja kwenda eneo
Jingine”alizidi kusema Jaji Hamid
Aidha,Jaji Hamidi alisema uboreshaji wa
Daftari la kudumu la wapiga kura
utahusisha wapiga kura utahusisha wapiga kura wote wapya na wazamani na
kwa wapiga kura wapya wataawaandisha wenye umri wa miaka 17 ambao mwakani
watafikisha miaka 18 ambao kisheria watakuwa wamefikisha umri wa kupiga kura
kikatiba
Vilevile Jaji Hamid akatoa wito kwa
Wananchi wote wenye sifa ya kujiaandikisha kujitokeza kwa wingi kwenye vituo
vya Uandikishaji Daftari la wapiga kura, vitakavyotangazwa
Kwa upande Kaimu Katibu mkuu wa
Tume ya Taifa tume ya Uchaguzi Dokta Sisti Cariah alisema mfumo huu mpya ni
mfumo bora tofautisha na ule wa kwanza kwani utarahisisha na kuharakisha wakati
wa uandikishaji.
“Mfumo ni
mzuri sana kwani ukishajiaandisha basi utapata hapo hapo kitamburisho chako cha
kupigia kura na utaondoa lawama za wananchi kulaumu tume ya uchaguzi”alisema
Dokta Cariah
Dokta Cariah alizidi kusema kwa sasa
serikali imeshawapa bilioni 15 ili kuweza kuanza mchakato wa uboreshaji na mchakato
mzima utagharamia bilioni 290.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni