WANAFUNZI WALIOKOSA MIKOPO WAFANYA KUFURU WIZARA YA ELIMU,WENGINE WAANGUA KILIO.SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na Karoli
Vinsent
KATIKA hali
isiyokuwa ya kawaida leo watendaji wa Wizara ya Elimu makao makuu wameonja joto
la jiwe baada ya Mamia ya wanafunzi wapya wa Masomo ya mwaka wa masomo 2014-2015 kuzizingila ofisi za wizara
hiyo kwa kile wanachodai kunyimwa pesa
za chuo na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu HESLB huku wengi wao wakisema
wakitoka kwenye Familia masikini.
Hayo yameibuka
leo kwenye makao makuu ya Wizara ya elimu zilizopo Posta Jijini Dar es Salaam
jirani na Ikulu ya Rais,ambapo Mwandishi wa mtandao huu alifika Wizarani hapo
majira ya mchana na kukuta mamia ya vijana wakiwa wamezizonga ofisi hizo huko
wanalalamika kwa kitendo cha kutopewa mkopo na Serikali.
Mwanafunzi mmoja aliyejitambulisha kwa
Jina moja la John ambaye amechaguliwa Chuo Kikuu cha Mlimani huku akizungumza
kwa uchungu sana alisema kwasasa haoni taswira yake ya masomo kutokana na bodi
ya Mkopo kumyima pesa za masomo pamoja na za kujikimu.
“Da sijui twenda wapi sisi watoto wa
masinikini hili taifa mimi ni yatima sina baba wala mama nimesoma kwanzia
msingi mapaka kidato cha sita kwenye shule za serikali tena za kata nashangaa
leo naingia chuo kikuu nanyimwa mkopo eti bodi wanasema mimi Bajeti aitoshi sasa sijui nitafanyaje mimi”alisema mwanafunzi
huyo aliyetambulika kwa jina moja la John.
Naye mwanafunzi mwengine ambaye
amechaguliwa Chuo kikuu cha Ualimu cha Duce alisema ameshangaa sana kwa Bodi ya
mkopo pamoja na tume ya Vyuo Vikuu nchini TCU kuwadanganya na pia kuipuuza
kauli ya waziri wa Elimu aliyosema kwamba wanafunzi wote waliomba kwenye masomo
ya kipaumbele kama walimu wapewe mkopo,badala yake Bodi hiyo imewanyima
wanafunzi waliomba kozi za ualimu na kuwapa wanafunzi wengine waliomba masomo
yasiyokuwa ya kipaumbele.
Mwengine alisikika akisema“Leo bunge la
katiba limetumia mabilioni ya fedha kwenye jambo ambalo wote kwa pamoja
tumekuwa mashahidi mchakato ule ulivyokuwa,harafu leo sisi watoto wamasikini
tunashindwa kusoma harafu mabilioni yetu
yamepotelea kwenye mchakato wa katiba mpya sijue twende wapi jamani hili taifa
hatuoni kama haoa kuna uongozi bora tumechoka”alisema mwanafuzi mwengine
Vilevile wakati wanafunzi hao wakipiga
kelele nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Elimu huku wakishinikiza kuonana na
Waziri wa Elimu na Mafunzo Shukulu Kawambwa ili kumwelezea hali ilivyo,nje ya
eneo hilo kulikuwa tayari Jeshi la polisi lilifika katika eno hilo ambalo lipo
jirani na ikulu ili kuweka ulinzi na kuwataka wanafunzi hao waandike majina
yote kwenye karatasi na majina hayo yapelekwe kwa Katibu wa Wizara hiyo.
Wakati wanafunzi hao wakiandika majina
ofisa Mmoja wa usalama aliyekuwepo ambaye akutaka jina lake litajwe mtandaoni
alimwambia mwandishi wa mtandao huu kwamba serikali inaandaa bomu ambalo
litakuja kuletea matatizo mbeleni kwani mataifa mengi amani yake imeharibika
ilitokana na viongozi kama wa sasa kupuuza kelele za wananchi na huko kupoteza
pesa kwenye mambo ambayo yasiyo ya msingi ikiwemo kwenye Bunge la katiba ambalo
mwisho wa siku pesa zimepotea bure.
Juhudi za kuwatafuta viongozi wa
Wizara hiyo ili kuzungumzi sakata hilo ziligonga mwamba kutokana viongozi hao
kutokuwepo ofisini na simu zao zilipopigwa hazikupatikana.
Kuibuka kwa wanafunzi hao kunakuja siku
chacha baada ya Bodi ya Mkopo nchini HESLB kutangaza majina ya wanafunzi waliopata
mkopo mwaka wa masomo 2014-2015 ambapo kati ya wanafunzi 57860 waliomba kwa
mwaka huu bodi hiyo imewapa wanafunzi 30654 tu na kusema serikali inauwezo wa
kuwakopesha wanafunzi hao tu kwakuwa Bajeti iliyotengwa na serikali ni ndogo
kuwapa wanafunzi wote mkopo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni