SAKATA LA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KUWA HOI,SSRA YASEMA UKWELI WA MAMBO ULIVYO SOMA HAPA KUJUA
Na Karoli
Vinsent
SERIKALI
nchini imesema hali ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii hipo salama na kusema habari
zozote zinazosemwa juu Mifuko hiyo
kuwepo katika hali mbaya ni za uongo na zenye nia ya kuchonganisha serikali na wananchi.
Kauli hiyo ya Serikali inakuja siku
chache baada ya magazeti nchini kuripoti kwamba hali ya mifuko ya Jamii hipo
katika hali mbaya na kusema chanzo cha
mifuko hiyo kuwa katika hali mbaya , kumetokana na serikali kukopa fedha
nyingi na kushindwa kurudisha na kupelekea mifuko hiyo kuishiwa fedha
Akikanusha Taarifa hizo leo Jijini Dar
es Salaam Mkuu wa uhusiano na
uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii (SSRA) Be Sarah Kibonde Msika wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari ambapo alisema SSRA inasikitishwa na taarifa zinazopotosha
juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwataka wananchi wazipuuzie taarifa hizo
kwani mifuko ya jamii ipo katika hali nzuri sana.
“Nawatoa hofu watanzania wate
waliosikia kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii ipo katika hali mbaya kwani mifuko
hiyo hipo vizuri na kwa sasa serikali
imeboresha maslahi ya wanachama kwenye mifuko hii na wengi wamekuwa wakipigia
kelele hii sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii na kusema inawaibia wanachama sio kweli,”
“ kwani wanachama wa mfuko
wa NSSF,PSPF ambao waliokuwa wakilipwa asilimia 65 kwa sasa watakuwa wanalipwa
zaidi ya asilimi 70 watakapo staafu,kwahiyo mifuko hii ipo katika hali nzuri tu”alisema
Msika
Be Msika alizidi kusema wanachama
walioko kwenye mifuko mingine ya hifadhi ya Jamii ikiwemo LPF,PPF watakapo
staafu watalipwa pesa zao kwa kutumia mfumo wa zamani na kuongeza kuwa
wanachama wapya waliojiunga kwaania mwenzi wa saba mwaka huu watatumi mfumo
mpya ambao ni wafaida zaidi na kuwaongezea kipato.
Naye mkurugenzi wa Huduma za sheria
kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)
Bwn Ngabo Ibrahimu alisema watanzania wazipuuze taarifa hizo na kusema ni jambo
la ajabu sana mtu unavyosema mifuko ya hifadhi ya Jamii hipo katika hali mbaya
wakati mifuko hiyohiyo imeongeza thamani ya pesa kwanachama wake,maana kitendo
cha kuongeza fedha kwanachama wake ni kwamba mifuko hipo katika hali nzuri.
Kuhusu Madai ya mradi wa ujenzi wa
chuo kikuu cha Dodoma na chuo hicho kutorudisha serikalini,
Mkurugenzi huyo wa Sheria
kutoka mamlaka hiyo alisema mpango wa ujenzi wa chuo cha Dodoma ni mpango wa
kuboresha elimu nchini na madai ya kusema chuo hicho kimeshindwa kulejesha
fedha serikalini ni uzushi wa watu wasiotaka kufuatilia mambo kwani fedha
zimeaanza kurudi serikalini kupitia chuo hicho.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni