TAMWA--VIJANA WENGI NI WALEVI KUPITA KIASI,UTAFITI WASEMA TATIZO LA AJIRA LAWA SABABU SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na Karoli
Vinsent
Kile
kinachoonekana Nguvu kazi ya Taifa inazidi kupungua kutokana na Vijana wengi
nchini Kujiingiingiza kwenye tabia unywaji pombe kupita kiasi na Kuacha kufanya
Shughuli za Maendeleo na kupeleka vijana kuishia kwenye Umasikini uliopitiliza.
Hayo yamegundulika Leo jijini Dar Es
Salaam wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti iliyoandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari wanawanke nchini (TAMWA) ambapo ripoti hiyo ya Utafiti imehusisha
kata tatu ikiwemo Makumbushao,Wazo,Tarakea zote zilizopo katika Manispaa ya
Kinondoni Jijini dar Es Salaam na lengo la utafiti huo ni kuangalia Jinsi gani
Pombe inavyoweza kuleta unyasaji wa Kijinsia.
Akisoma Ripoti hiyo ya Utafiti mbele ya
Waandishi wa habari, Mhadhili Mwandamizi wa Elimu ya Biashara kutoka Chuo Kikuu
cha Dar Es Salaam Dk Severine kessy,
Alisema utafiti huo umebaini Vijana wengi
katika Sehemu hizo wameendekeza unywaji pombe na kuacha kujikita katika masuala
ya Maendeleo.
“Utafiti wetu umeangalia Jinsi gani
pombe inaweza kuleta athari katika Jamii, katika kata hizi tatu za Makumbusho,wazo Tarakia,tumegundua
Vijana wengi wanatumia vilevi mda wote na Kilevi ambacho wanakitumia sana na
Pombe aina ya Kiroba huku wakiaacha kufanya mambo ya Maendeleo”
“Na kila
tulipokwenda katika Kata hizo tumekuta watu wanakunywa Pombe kupita kiasi huku
wengine wakitembea nazo mfukoni na hata upatikanaji wa pombe yenyewe
zinapatikana kirahisi kwani zipo mita mia tu kutoka kwenye makazi ya watu na
matokeo yake unyasaji wa Kijinsia”alisema Dk Kessy.
Dk Kessy alizidi kusema utafiti huo
umebaini kila Rika yaani kwaanzia Vijana
mpaka wazee wamekuwa wahanga wa Unywaji pombe.
Aidha Dk Kessy alisema Utafiti
umegundua sababu ya Vijana wengi kujikita katika Unywaji wa Pombe uliopitiliza
na kusema sababu kubwa ni Tatizo la Ajira na msongo wa Mawazo na kuongeza
Matizo mengi sana ya Unyanyasaji wa kijinsia umetekona na Unywaji pombe
uliopitiliza.
pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi Wa habari TAMWA Be Gladness Munuo picha na Maktaba |
Kwa upande wake kaimu
mkurugenzi wa chama hicho cha habari, Bi. Gladness Munuo Aliitaka Jamii kuachana unywaji Pombe na kuwataka Vijana wajikite kwenye masuala ya
Maendeleo na kuliletea Taifa Maendeleo huku ikizingatiwa Vijana ndio moyo wa
Taifa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni