siku ya mtoto wa kike dunia=Mtandao wa kupinga ndoa za utotoni wafanya makubwa Dar
Tunacheza, watoto wakiwajibika katika siku hiyo muhimu katika ofisi za KIHOWEDE zilizopo jijini Daresalaam |
Waandishi wa habari wakiwa makini kuuhabarisha umma kuhusiana na siku hiyo ya mtoto wa kike duniani. Watanzania wametakiwa kuachana na mila potofu ambazo ni kandamizi kwa mtoto wa kike. |
Imeelezwa kuwa mtoto wa kike bado yuko katika wakati mgumu wa kuendelea kupata fursa za elimu kutokana na ukweli kuwa mtoto huyo ameendelea kubaguliwa tokea katika ngazi ya familia kitendo ambacho kinaendeleza ule utamaduni wa wanawake kuwa tegemezi wa wanaume,
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, Mwenyekiti wa mtandao wa kupiga vita ndoa za utotoni TCEMN Justa Mwaituka amesema hapa Tanzania bado hali si shwari kwani matendo ya kumbagua mtoto wa kike yanaendelea kukua kwa kasi ya kimbunga,
Mwaituka ameendelea kusema kuwa Mtoto wa kike ameendelea kubaguliwa tokea ngazi ya familia, wanaozesha mapema ili fedha ipatikane kaka yake akasome huko ni unyanyasaji wa mtoto wa kike aliongeza,
Mtandao huo wa kupiga vita ndoa za utotoni ulianzishwa rasmi mwaka 2012 ukiwa na jumla ya mashirika 35 ambao kwa pamoja wamelenga kuhakikisha mtoto wa kike naye anapata fursa saawa na yule wa kiume, wakisema ukimuelimisha mwanamke utakuwa umeelimisha taifa.
Katika kipindi chao chote tokea kuanzishwa kwa mtandao huo, inadaiwa bado mtoto wa kike ameendelea kukandamizwa kwa kunyimwa fursa za kupata Elimu Bora, huduma za afya, na lishe bora, haki ya kupata msaada wa kisheria,ulinzi dhiodi ya Ubaguzi,unyanyasaji na vitendo vingine vyote vya unyanyasaji wa kijinsia na usafirishaji haramu wa watoto hususani watoto wa kike.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni