Zinazobamba

HABARI NZITO LEO--KURA FEKI NYINGINE KWA UPANDE WA ZANZIBAR YAGUNDULIKA,JUKATA LAMBANA SITTA



Na Karoli Vinsent
KILE alichokiona amefanya siri kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta kuchakachua Thuluthi 2 upande wa Zanzibar ili kupitisha Rasimu iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba sasa Siri hiyo imeanza kufichukua.
          Baada ya Jukwaa la Katiba nchini JUKATA  limefichua  hujuma nyingine ya Thulithi 2 kwa upande wa Zanzazibar baada ya kubaini kuorodheshwa kwa Mjumbe wa Bunge hilo kutoka Tanzania bara ambaye jina lake limeorodheshwa kwa majina ya wapiga kura kwa upande wa Zanzibar.
          Mujumbe huyo ni Zakhia Meghji ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya   Chama cha Mapinduzi CCM ambapo amepiga kura  kwa wajumbe wa Upande wa Zanzibar wakati yeye anatambulika kwamba ni mjumbe wa Tanzania bara.
          Kufichuliwa kwa Siri hiyo na Jukwaa la katiba nchini  juu ya uchakachuaji wa theluthi 2 kwa upande zanzibar umekuja siku chache baada ya chama cha NCCR Mageuzi kubaini kuorodheshwa kwa mjumbe kutoka chama hicho kwa upande wa Zanzibar kupiga kura ya ndio wakati hakushiriki vikao vya bunge maalum la katiba.
            Akifichua Hujuma hiyo leo Jijini Dar ES Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba nchini JUKATA Deus Kibamba wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kibamba akizungumza kwa hisia alisema  kwamba wamechunguza wameibani kuorodheshwa Zakhia Meghji ambaye ni Mjumbe kutoka Tanzania bara kupiga kura ya ndio kwa upande wa Zanzibar.
            “Jukwaa la katiba limebaini kuwapo kwa mjumbe mwingine feki kwa upande wa Zanzibar Zakhia Meghji ambaye  ameorodheshwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Bunge la Maalum la katiba namba 149  kwamba ni mjumbe wa Zanzibar na kapiga kura ya ndio wakati yeye anajulikana wazi ni mjumbe wa Tanzania bara wakati  mjumbe huyo kupitia Gazeti la Serikali la mwezi julai lilimtaja Zakhia Meghji kuwa ni mjumbe Tanzania bara inakuweje leo tena wakati wa kupiga kura  atambulike kwamba ni  mjumbe wa Zanzibar yote haya ni kufanya hujuma ili kupata thelusi 2“Alisema Kibamba .
         Kibamba alizidi kusema kwa ishara hiyo ni wazi Theluthi 2 haikupatikana bali Samwel Sitta na wenzake walifanya uchakachuaji wa makusudi ili kupisha katiba yao na kusema hizo kura mbili zilizopitisha kura kwa upande wa Zanzanibar ni wazi ni uongo wa wazi kwani mapaka sasa kura mbili tayari zimebainika ni feki.
           Aliongeza kuwa kwa sasa Jukwaa la katiba baada ya kuona uchakachuaji huo wameipa kazi kampuni iliyobobea kufanya uchunguzi kwenye kura za ndio kwa upande wa Zanzibar ili kujua ukweli na wakibaini tena kama kuna uchakachuaji mwengine basi hawatasita kuchukua hatua kali.
             Aidha Kibamba alisema  JUKATA wamesikitishwa sana  na kitendo cha Bunge Maalum la Katiba kuyazika kwa kiasi kikubwa maoni ya wananchi kwa kitendo cha kuondoa Mamlaka na madaraka ya Wananchi,maadili na mikio ya uongozi na utashi kwa umma na kuzidi kuendelea Tanganyika kuvaa koti la Muungano.
            Ambapo alisema kwa sasa Jukwaa la katiba Linajipanga kusambaza Rasimu ya katiba iliyopendekezwa na bunge maalum nchi nzima ili wananchi waamue ukweli juu ya katiba.
        Vilevile JUKATA limewataka watanzania kusoma kwa umakini Katiba iliyopendekezwa na bunge iliwaweze kujua ukweli.  





Hakuna maoni