Zinazobamba

HABARI NYINGINE KALI KUTOKA BANK YA FNB

 FNB Logo
Dar es Salaam: Oktober 22, 2014. 
 Wafanyabiashara na wateja wa First National Bank (FNB) sasa wanapata huduma za Premier Banking zinazotolewa katika kitengo maalumu kilichopo tawi la Peninsula jijini Dar es Salaam.

Kupitia kitengo hicho wateja, sasa wateja watahudumiwa  na watoa huduma maalum wakiongozwa na meneja wa kitengo hicho, na kupata huduma za utunzaji, usimamizi wa fedha na uwekezaji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kitengo hicho, Afisa Mtendaji Mkuu wa First National Bank, Dave Aitken alisema “Tunafurahi kuzindua kitengo hiki maalumu kwa wateja wetu ambacho kitakuwa na huduma maalum za kibenki pamoja na kutoa ushauri kwa wateja. Tunaamini wateja wetu hawafanani kwa mahitaji yao na tutatoa huduma zinazokidhi mahitaji kama inavyoendana na falsafa yetu “Tukusadieje?”.

Alisema kutokana na matokeo ya ukuaji wa uchumi Tanzania kwa miaka kadhaa, mahitaji ya wateja wa benki yameongezeka na FNB imekuja na ufumbuzi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hizo, kwa kuwekeza katika kitengo cha Premier Banking ili kusaidia kukidhi mahitaji ya wateja.


Uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia 7 kwa miaka kadhaa, na uchumi wetu sasa unatumiwa na Benki ya Dunia  kama kigezo cha mabadiliko ya uchumi Afrika Mashariki. Wachangiaji wakubwa wa ukuaji wa uchumi ni wazalishaji, wafanyabiashara, taasisi za kifedha, sekta ya mawasiliano na masuala ya ujenzi ambapo ulionyesha ukuaji mkubwa zaidi wa asilimia 8.0 kwa mwaka 2012.

“Matokeo ya ukuaji huu wa uchumi huonekana katika misingi inayochangia ukuaji wa kiwango kikubwa cha sekta ya biashara. Wateja wa sekta hiyo sasa wanahitaji ufumbuzi wa kitaalam katika huduma za kifedha na sasa kitengo cha FNB Premier Banking kitatatua changamoto hizo na kuchangia ukuaji wa uchumi" alisema Aitken.
Huduma za kisasa za kiteknolojia za First National Bank, huwezesha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa urahisi kupitia kompyuta na simu za mkononi ambazo ni huduma za kimataifa na zenye usalama wa hali ya juu.

FNB ina malengo makubwa ya kuendeleza maendeleo ya sekta ya fedha  Tanzania na imelenga kuleta uzoefu na ubunifu wao wa huduma za kibenki kutoka kanda ya sahara Afrika katika sekta mbalimbali na kushiriki katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Hapa Afrika, benki ya First National Bank ilianzishwa mwaka 1874 na ina matawi Zambia, Msumbiji, Lesotho, Swaziland, Botswana na Namibia na makao makuu  yapo Afrika Kusini. FNB imelenga kuwa benki inayo aminika zaidi Afrika.

Benki ya FNB Tanzania ilianzishwa mwaka 2011 na matawi ya benki yapo Posta, Quality Centre, Peninsula, Kariakoo na Kimweri Dar as Salaam. Kwa taarifa zaidi tembelea www.fnbtanzania.co.tz au tovuti info@fnb.co.tz



                                                                MWISHO



Kind regard,
HYASINTA TIMOTHY