HABARI KUBWA LEO--DOKTA SLAA ALIPUKA NA ASEMA MAZITO NI KWA TANZANIA KUNYIMWA MISAADA NA WAHISANI, SOMA HAPA
Na Karoli
Vinsent
HUKU ikiwa
nchi Wahisani hususani Uingereza,Swiden na zengine zikiwa zimesitisha Misaada
kwa Serikali ya Tanzania kwa kile wanachodai ni kuchoshwa na Vitendo vya
Ufisadi vinavyofanywa na Watendaji wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwenye Akaunti ya Escrow ambapo zaidi ya
Bilioni 400 zimeibiwa.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa ameibuka na kumvaa Rais jakaya Kikwete
na kusema yeye ndio anafaa kurahumiwa na Watanzania kwa kitendo chake cha kuwakumbatia
mafisadi ndani ya serikali yake na kushindwa kuwachukilia hatua.
Hayo yamesemwa Mda huu wakati wa Mahojiano kati ya Mwandishi
wa Mtandao huu na Katibu huyo Mkuu wa Chadema Dokta Wibroad Slaa,ambapo amesema
kuhusu kitendo cha nchi wahisani ambao wamekuwa wakuisaidia Tanzania kufanya
maamuzi hayo,yanatokana na Rais Kikwete kuwakumbatia mafisadi hata wakati wa
kampeni za Uchaguzi mwaka 2010 aliwanadi kwa wananchi ili washike uongozi.
“Wahisani mpaka wamefikia hapo na
wamechoka kama sisi tulivyo choka na ufisadi kwani hata hizo pesa zinazoliwa
zinatokana na kodi za nchi yao, na nchi yeyote inayojali pesa za walipa kodi
haiwezi kufanya hata siku moja kama wanavyofanya serikali hii,na haya yote ni uzembe ambayo Unatokana
na kuongozwa na viongozi wasiokuwa na hofu ya mwenyezi Mungu na wala suala la
ufisadi Tanzania sio geni kwani ni utamaduni usiozoeleka”alisema Dokta Slaa
Dokta Slaa alizidi kusema kwa uchungu kwamba Watanzani
wataumia mara mbili kwanza ni kwakukosasa fedha za Maendeleo kutoka kwa marafiki
wahisani na pili fedha zimepotea na kutokana na ufisadi, na amesema kuwa Ufisadi huo wa Akaunti ya Esrow unatokana na Serikali kuwa jueri na inatokana na kuwepo kwa serikali
ambayo inawalinda mafisadi na kutowachukulia hatua mafisadi,
Vilevile Dokta Slaa alimtupia Lawama
Spika wa Bunge la Muungano Anna Makinda kwa kitendo chake cha kuwapuuza wabunge
wa upinzania ambao walitaka iundwe tume maalum ili kuchunguza sakata ka ufisadi
kwenye Akaunti ya Escrow ambapo Dokta slaa alisema kuto kufanywa hivyo kwa
spika ni wazi ni kulinda mafisadi.
Kuhusu misamaha ya kodi inayotolewa na
serikali ambayo imefikia trillion 1.5
Dokta Slaa alisema angekubaliana na serikali
kwamba ingewasemehe mama lishe au watanzania masikini lakini anashangaa kwanini
serikali inawasemehe makampuni makubwa kodi ambayo yanaingiza mamilioni ya
fedha na kusema kitendo cha serikali kusamehe kodi kutazidi kuifanya Tanzania
kuwa masikini.
Kuhusu
ununuzi wa Hedkopta ya jeshi ambayo umelenga kwa ajiri ya uchaguzi ndani ya ccm
mwakani
Slaa alisema yeye mwenyewe amekamata barua
ambayo ilitoka jeshini kwenda kwa nchi
ya Ufaransa na kusema barua hiyo imeonesha ubabaishaji mtupu
“Serikali
yetu inanunua hedkopta kutoka ufaransa kwa njia ya ufisadi,ambao ufadi huu
unafanana na ule wa kununua ndege ya Rais pamoja na rada,kwanza kununua
hedkopta kwa ajiri ya jeshi letu ni jambo jema,lakini lugha iliyotumika kwenye
barua niliyoikamata sio nzuri kwani imesema hivi kwamba hizo hedkopta zifike
kabla ya uchaguzi mkuu kwahiyo jina la
jeshi linatumika kwa ajiri ya kukisaidia chama cha mapinduzi”alisema Dokta Slaa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni