HABARI KUBWA LEO--MAZITO YAIBUKA KUHUSU THELUTHI 2 YA ZANZIBAR,KUMBE MJUMBE WA UKAWA ALITAJWA KUPIGA KURA KUMBE NI FEKI, NAYE MBATIA AMKABA SITTA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na Karoli
Vinsent
HUJUMA
alizofanya Aliyekuwa mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta wakati
wa Kupata Theluthi 2 kwa Upande wa Zanzibar ili kupitisha Rasimu ya katiba
iliyopendekezwa na Bunge,sasa hujuma hizo zaanza kufichuka,
Baada ya Chama
Cha NCCR mageuzi kuibuka na kufichua hujuma iliyofanywa na Samwel Sitta
kutokana na kumuorodhesha Mjumbe Bunge hilo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa
chama Cha NCCR-Mageuzi Zanzibar Ndugu Haji Ambar Khamis kuwa Miongozi mwa
wajumbe walioshiriki kupitisha katiba hiyo iliyipendekezwa huko yeye akuwepo
wala akushiriki vikao hivyo.
Hayo yameibuliwa mda huu Jijini Dar
Es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia wakati wa
Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Mbatia alisema chama hicho ilipopata
taarifa za kuorodhesha kwa Mjumbe huyo kuhusu kupitisha Rasimu ya Bunge ndipo
wakafanya uchunguzi ikiwemo na kumwita Ndugu Haji Ambar Khamisi ili kupata
ukweli.
“Tumechunguza na Kubaini kwamba Ndugu Haji Khamis,ametuthibitishia kwa dhati
kwamba hakuwahi kushiriki katika kuandaa wala kupitisha katiba iliyopedekezwa
tangu bunge hilo liliporejea kwa mara ya pili tarehe 05 Agosti 2014.”
“ Na
kitendao cha kuandika jina la kiongozi wetu wa Taifa katika katiba
iliyopendekezwa bila ridhaa yake ni ulaghai uliokithiri kwa watanzania na Dunia
kwa ujumla kwani kitendo hicho ni cha udhalilishaji kwa yeye binafisi,Familia
yake chama chetu pamoja na viongozi wanachama wote wa Umoja wa kutetea katiba
ya wanachi UKAWA na watanzania”Alisema Mbatia.
Mbatia alizidi kusema chama hicho
kimeamini kitendo hicho kimefanywa kwa makusidi na Viongozi wakuu wa Bunge
Maalum la Katiba ili kukidhi haja zao Binafsi na kulaghai umma wa Watanzania na
kusema ni ishara hatarishi kwa usalama wa Taifa letu kwani kitendo hicho
kinaweza kusababisha machafuko.
Aliongeza kuwa Uongozi wa NCCR-Mageuzi
umepokea katiba iliyopendekezwa kwa Fedheha na Mshtuko mkubwa na kuamini kuwa
kuna mkakati mbaya wa kusambaratisha chama hicho kinachokua kwa kasi nchini.
Aidha,Mbatia alisema kwa sasa Chama
chake hakitaweza kuvumilia uongo na Uzushi aliufanya mwenyikiti wa Bunge Maalum
La katiba katika kupata Thelusi 2 kwa upande wa Zanzibar kwa kufoji wajumbe
ambao hawakuwepo kwenye bunge hilo na kusema kwa sasa chama hicho tayari
kimewasiliana na wanasheria ili kwenda mahakamaini ili hujuma hiyo igundulike.
Kwa upande wake ndugu Haji Ambar
Khamis alisema anashangaa sana kwa kutajwa katika wajumbe walioshiriki kupiga
kura kuipitisha rasimu ya bunge na kusema hajawai kuwepo wala kushiriki katika
bunge hilo.
“Yaani nashangaa sana maana nimekuwa
siishi kwa raha napigiwa simu za vitisho kutoka sehumu mbalimbali na kusema
ukweli jamini mimi sijawai kuwepo kwenye Bunge la katiba tangu tulivyosusia vikao
hivyo na huu umoja wetu wa UKAWA nashangaa sana leo natajwa mimi kuwepo jamani
huu ni uongo mkubwa sana mimi sikuwepo”alisema Khamisi
pichani ni Makamu Mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI Zanzibara Haji Khamis |
Katika hali isiyokuwa ya Kawaida Wakati
Haji Ambar Khamisi akiwa akijielezea alishindwa kabisa na kuanza kulia na
kusema Familia yake ipo katika hali mbaya pamoja na yeye kutokana na hali ya kisiasa Visiwani
Zanzibar kuanza kuchafuka na uwenda familia yake ikauliwa.
Baada ya kusema maneno hali ikazidi
kuwa mbaya na akapata mshutuko huku kikao hicho na Waandishi wa Habari
kikasimamisha na Viongozi wa chama hicho waliokuwepo mkutanoni hapo wakamkimbiza Haraka Hospitali ya Amana iliyoko Jijini hapa ili kupata Matibabu.
Baada ya Hali hiyo kutokea ndipo
Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia aliitaka Serikali impe ulinzi Mjumbe
huyo huku ikizingatia undani wa suala lenyewe na akakumbushia Mauaji ya
Kikatili na yakinyama aliyofanyiwa aliyekuwa mjumbe wa iliyokuwa tume ya
marekebisho ya katiba Marehemu Dkt Edmund Mvungi na kusema uwenda unyama huo
ukamkuta makumu huyo mwenyekiti.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni