LHRC WAJITOSA MGOGORO WA KATIBA, WATAKA SERIKALI IINGILIE KATI ILI KUSURU MCHAKATO,
Mwenyekiti wa kamati hiyo maaluum ya katiba akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaamKituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kamati yake maalum ya katiba SCOC imeitaka mamlaka ya juu ya nchi kuupa kipaumbele mgogoro ambao umetokea kwenye bunge maalum la katiba ili kunusuru mchakato wa kupata katiba mpya.
Hayo yamesemwa leo jijini dar es salaam na mwenyekiti wa kamati hiyo ya katiba Dkt KHOTI KAMANGA wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema kuwa kamati yake imesikitishwa sana na mwenyendo mbovu wa bunge maalum la katiba na hatimaye kuparanganyika kwa chombo hicho muhimu kilichokuwa na kazi ya kujadili na kuboresha rasimu ya katiba kama ilivyowakilishwa na tume ya mzee warioba.
Dkt KAMANGA amesema kuwa ili kuurudisha mchakato wa katiba katika mstaari ni lazima viongozi wa juu ya nchi huku akimtaja rais KIKWETE kuuchukulia mgogoro huo ambao umeligawa bunge maalum katika hali ya ukubwa na kutafuta mbinu za kuwapatanisha ili wale waliotoka bungeni
kurejea na kutafuta katiba mpya kwa pamoja. Aidha amesema kuwa ni lazima wabunge na watanzania wote kujenga utamaduni wa kusikilizana na kushauriana na kupokea ushauri ukiwemo ule unaotokana na wataalam na wazalendo bila kupuuzia mawazo yao kwani yapo yanayotaka kuunusuru mchakato huo,

Aidha katika hatua nyingine kamati hiyo imeshauri kwamba katika mchakato wa kupata katiba mpya ni lazima bunge lizingatie maoni ya wananchi yaliyopo ndani ya rasimu ya katiba na iwe ndio agenda kuu
tofauti na sasa ambapo misimamo ya vyama ndio imeonekana kujadiliwa sana kuliko rasimu yenyewe.
tofauti na sasa ambapo misimamo ya vyama ndio imeonekana kujadiliwa sana kuliko rasimu yenyewe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni