SERIKALI IMETUMIA ZAIDI YA BILIONI 111 KUNUNUA MAZAO
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bw. Charles akiongea na waandishi wa Habari( Hawapo
Pichani) kuhusu mafanikio yaliyopatikana na wakala hao ikiwamo kutumia Zaidi ya
Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha Mwaka 2013/2014.
wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mipango na Uendeshaji wa wakala huo
Bi. Anna Mapunda.
Baadhi ya waandishi wa Habari
waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa
wa Hifadhi ya Chakula Bw. Charles wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi
wa Idara ya Habari (fhb)
SERIKALI imetumia zaidi ya Shilingi
Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa
ni malipo kwa wakulima baada ya kuiuzia nafaka Serikali.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Charles Walwa wakati wa
mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa
akieleza mafanikio yaliyofikiwa na wakala huo.
Walwa alisema kuwa wakala huo
umeweza kuongeza kiasi cha nafaka zilizonunuliwa kutoka kwa wakulima kutoka
tani 61,587.784 mwaka 2008/2009 hadi tani 219,377.282 mwaka 2013/2014 ikiwa ni
matokeo ya kuboreshwa kwa mifumo ya utendaji wa wakala huo.
"Hadi kufikia Desemba 31 mwaka
2013 wakala ulinunua tani 219,377.282 za nafaka sawa na asilimia 110 ambapo
tani 218,878.600 ni mahindi na tani 498.682 ni mtama" alisema Walwa
.
Aliongeza kuwa wakala umeingia
makubaliano ya mashirikiano ( Memorandum of Understanding(MOU) na Shirika la
Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili kuwahakikiishia wakulima soko la uhakika.
Katika kutekeleza makubaliano na WFP
Walwa alisema kuwa wakala umeuza tani 80,000 mwaka 2011/2012 ambapo kwa sasa
wakala unaendelea kutekeleza mkataba mwingine wa kuuza tani 23,000 kwa mwaka
2013/2014.
Katika hatua nyingineWalwa alisema
kutokana na mfumo mzuri wa manunuzi ya nafaka kutoka kwa wananchi, ajira za
muda kwa wananchi takribani 3000 zizizalishwa na makundi mbalimbali ya wananchi
wakati wa kukusanya nafaka tatika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula umepanga kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 241,000 za Sasa
hadi tani laki 400,000 ifikapo mwaka 2016 na Tani 700,000 ifikapo mwaka 2024.
THE GOVERNMENT OFFICIAL BLOG
CHANZO,FULL SHANGWE.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni