Zinazobamba

Bodi ya TASAC:Tumejiridhisha na maboresho ya bandari za Kemondo na Bukoba.


*Yampongeza  Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za maboresho ya Bandari hizo

Na Mwandishi Wetu ,Bukoba

Bodi ya Wakurugenzi  wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya ujenzi wa Bandari za Kemondo na Bukoba hivyo fedha hizo zinatakiwa kuleta tija na zirudi kutokana huduma zitazotolewa na Bandari hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati ziara Bodi katika Bandari hizo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Nah.Mussa Mandia amesema kuwa baada ya maboresho ya miundombinu ya ujenzi wa bandari watahudumia mizigo na abiria kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.

Bodi hiyo ilitembelea Bandari ya Kemondo ,Bukoba pamoja na kiwanda cha  Vic Fish TASAC inadhibiti uzito kwa ajili ya Usafirishaji wa Samaki nje ya nchi.

Amessema kuwa fedha ya Bandari ya Kemondo bilioni 20 na ujenzi wake umekamilika ambapo huduma zake zimeongezeka hadi kufikia tani 150000 kwa mwezi na mapato yake yameongezeka mara tatu huku Bandari ya Bukoba ujenzi wake ukiwa katika hatua za mwisho unaogharimu zaidi ya sh.Bilioni 19.Amesema  kuwa kama wadhibiti ni kuhakikisha Bandari hizo zinaendelea kutoa huduma bora na tija kwa serikali huku akitaka wasimamizi wa bandari kusimamia kwa  weledi.

Amesema Serikali ya awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kutimiza ndoto katika upanuzi wa bandari za Kemondo na Bukoba ambayo miundombinu yake ilikuwa ya zamani ambapo haiendani na mahitaji ya sasa.Hata hivyo amesema kazi bodi itaendelea kushauri katika taasisi wanayoidhibiti ambapo matokeo yake yanaonekana kwa miradi mbalimbali kwenye bandari nchi nzima

Mkuu wa  Bandari ya Bukoba wa TPA Malick Ismail amesema kuwa Bandari hiyo maboresho ya ujenzi bandari hiyo baada ya kukamilika watahudumia meli nne kwa wakati mmoja tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wakihudumia meli moja.



Hakuna maoni