Mhagama awataka wakurugenzi wa elimu kuwapa ushirikiano walimu wapya, asema kutasaidia kuwafanya walimu hao kuona ni mikono salama ya kufanyia kazi
Na selemani Magari
Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh. Jenista mhagama, amewataka maafisa elimu, wakurugenzi wa elimu na wakuu wa Chuo kuwapokea kwa mikono miwili walimu wapya walipangiwa katika halmashauri zetu ili walimu hao wajione kama wamefika katika mikono iliyo salama katika kazi zao,
Akizungumza katika uzinduzi wa vitabu vya uchambuzi wa matokeo kwa kidato cha nne ya mwaka 2013, Mhagama amesema, serikali imewapangia jumla ya walimu 18093 katika halmashauri mbalimbali hapa nchini ambao kati yao walimu wa stashada ni 5416 na wale wa shahada ni 12677 wanaotarajiwa kuripoti kwa wakurugenzi kuanzia leo ili wapangiwe vituo za kufanyia kazi,
Mhagama amesema walimu hao wanatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa walimu unaolikuta taifa kwa shule zetu za kata na hata zile za misingi ambazo kwa mda mrefu kumeonekana uhaba wa walimu hao,
Wadau wakimsikiliza kwa makini naibu waziri alivyokuwa akiwataka kuwapokea kwa wema walimu wapya |
Amesema katika kuhakikisha Taifa linaboresha mfumo wake wa elimu kwa kuongeza ufanisi katika sekta hii, serikali imejipanga vizuri kuhakikisha walimu wanaoingia katika fani hii hawajutii uwepo wao, na kwa kuanzia tunawaomba maafisa elimu kutusaidia kwa kuwapokea walimu hao kwa mikono miwili ili wajione hawakukosea kusoma fani ya ualimu
Katika uzinduzi huo wa vitabu vya uchambuzi, Mhagama, alifanikiwa kugawa baadhi ya kopi za vitabu hivyo kwa Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu(ELIMU) Mh. Kassimu Majariwa
Naibu katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Bi Consolata Mgimba hapa nchini akifafanua baadhi ya mambo, |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni