Zinazobamba

BIdhaa zenye sumu zaingizwa kiholela nchini, Ofisi ya makamu wa rais haina taarifaa

Mratibu wa mtandao wa TOAM akionyesha bidhaa haramu zilizoingizwa nchini kimagendo toka nchini Afrika kusini, Bidhaa hizo zinadaiwa kuwa na madhara  makubwa kwa binadamu, hata hivyo ofisi ya makamu wa rais wakiri kutokuwa na taarifa ya kuingizwa bidhaa hizo za GMOs kimagendo

 Na SELEMANI MAGARI
Mtandao unashughulika na masuala ya mazingira hapa nchini umebaini uingizwaji holela wa Bidhaa za Gmos hapa nchini huku ofisi ya makumu wa rais ikili kutofahamu uingizwaji wa bidhaa hizo zinazotokana na kupandikizwa kwa vinasaba mbalimbali ambavyo ni hatari kwa afya ya binadamu, 

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, jiji Daresalaam, Mratibu wa mtandao wa mashirika yanayojishulisha na masuala ya mazingira, vyakula na kilimo hapa nchini, TOAM, Bw. Abdalah Ramadhani amekiri kuona uingizwaji wa bidhaa hiyo hapa nchini katika baadhi ya maduka yetu huku hakuna taarifa sahihi kama bidhaa hizo zimeruhusiwa rasmi kuingizwa katika soko la Tanzanai

Ramadhani amesema, wanashangazwa kuona wananchi wa kitanzania wakilazimishwa kulishwa bidhaa za GMO ambazo zimesadikiwa na wanasayansi maarufu duniani kuwa zina madhara makubwa kwa afya ya binadam,

Abdalla Ramadhani akifafanua madhala ya Bidhaa zinazotokana na GMOs kwa waandishi wa habarii, Ramadhani amesema bidhaa za GMOs Ni sumu kwa wananchi na hazikubaliki
Amesema, kuwa mpaka sasa, bidhaa za GMO zinazitofahamu kutokana na ukweli kuwa, wasambazaji wa bidhaa hizo kutokuwa tayari kuwajibika kama bidhaa hizo zitaleta matatizo kwa walaji kama sheria yetu ya mazingira namba 56(1) inavyowataka na badala yake wamekua wakiishinikiza serikali kuangalia namna ya kuibadilisha kanuni hiyo ili waweze kuingiza bidhaa hizo kwa urahisi,

Aidha katika hatua nyingine, Mratibu wa mtandao wa TOM ameitaka serikali kuitisha mjadala wa wazi wa wananchi kujadili madhara na faida za bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia vinasaba ili kuwapa fursa wananchi wenyewe kuamua kama bidhaa hizo zitumike katika masoko yetu au la,
Sambamba na hayo Ramadhani  ameiomba serikali kuasimama katika msimamo wake wa kuwalinda walaji kwa kutobadili kipengele cha sheria namba 56(1), kwani kipengere hiko ni muhimu sana kwa afya ya watanzana na kizazi  kijacho

Akizungumzia utafiti uliofanywa na wanasayansi mbalimbali dunia kuhusiana na bidhaa zinazozalishwa kwa kuongezea vinasaba, Mkurugenzi mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali  ya Tanzania alliance for biodivesity,  (TABIO) Michael Farrelly amesema hali ilivyo ni kwamba bidhaa za GMOs zimeonyesha madhara makubwa kwa wanyama waliowafanyia uchunguzi, hivyo ni hatari kama bidhaa hzio zikitumika kwa binadamu,
 Amesema jopo la wataalam zaidi ya 300 walimfanyia uchunguzi panya kwa kumlisha vyakula vilivyozalishwa kwa vinasaba mbalimbali kwa muda wa miaka miwili na utafiti huo umeonyesha wazi madhala makubwa kwa mnyama huo kwa kipindi cha muda mfupi

Aidha, Mtaalamu huyo toka asasi ya TABIO, amewashauri wananchi kujenga tabia ya kuchunguza nembo ya vyakula wanavyonunua kabla ya kuvitumia ili kujua kama bidhaa hizo zimezalishwa kwa vinasaba vya GMOs,

"Tunawaasa watanzania kujenga tabia ya kuangalia bidhaa wanazozinunua kabla ya kuzitumia maana tayari, bidhaa za GMOs zimeanza kuingizwa katika soko la Tanzania kiholela sasa kunauwezekano wa kulishwa sumu kutokana na bidhaa hizo"Aliongeza Bw. Farrelly

Hakuna maoni