LHRC CHAWAPIGIA MAGOTI SERIKALI,KISA NI UTAPELI UNAOFANYWA WAKOPESHA FEDHA DHIDI YA WAJASILIAMALI,
Kile kinachodaiwa kuwa ni dhuruma , wizi na utapeli
uliokithiri unaofanywa na taasisi za kukopesha fedha hapa nchini umewasukuma kituo cha sheria na haki za binadam kuitaka serikali kuandaa mazingira ya kuwadhibiti taasisi hizo
ili wasiweze kuendelea kuwatapeli maaelfu ya wajasiliamali,
Hatua hiyo imekuja kufuatia viliyo vya wajasiliamali katika
mikoa ya Arusha, Meru na Babati ambao wamekusanya zaidi ya kesi 26 katika kituo
Cha arusha wakiwatuhusu mashirika hayo yanayojihusisha na ukopeshaji wa fedha
kufanya utapeli wa waziwazi kwa raia hao,
Akizungumza na waandish wa habari mapema hii leo, Kaimu
mkurugenzi wa mradi wa kazi za staha kwa wananchi waliojiari katika sekta
zisizo rasmi, Adv. Flaviana Charles amesma katika mradi huo wamegundua uatapeli
wa hali ya juu unaofanywa na mashirika yanaojihusisha na kukopesha fedha kwa
wananchi, huku utapeli mkubwa ukifanywa kwa njia ya mikataba ya kinyonyaji,
Charles, ameendelea kufunguka kuwa,katika mradi huo uliowashirikisha
jumla ya wajasiliamali 775, umeonyesha mafanikio makubwa sana kwa kubaini
changamoto mbalimbali za
wajasiliamali, ambazo kama serikali hatakuwa makini
nazo basi tunatengeza bomu kubwa ambalo likifumka hakuna atakae pona,
Mradi huoa ulitumia kipindi cha miaka mitatu katika mikoa
hiyo ya kanda za kaskazini, umebaini uhitaji wa hali ya juu kwa nguvu za
serikali kuingilia kati mifumo mibovu ya
taasisi za kukopesha fedha ambayo imekuwa ikiwanyonya wajasiliamali hapa
nchini,
Katika kuondoa tatizo la utapeli linalofanywa na taasisi za
kifedha ambazo zimepewa dhamana ya kukopesha wajasiliamali, Kituo kimependekeza
uundwaji wa haraka wa mamlaka ya
kuthibiti taasisi za mikopo hapa nchini, ili mashirika ya mikopo waweze kutoa
mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi kwa wajasiliamali wa kitanzania
Watu wamekuwa wakitapeliwa, na unakuta taasisi zingine
hazijasajiriwa kabisa, lakini bado zinaendesha shughuli za ukopeshaji na hata
zile ambazo zimesajiriwa bado zinatengeneza mikata ambao ni mizito kuisoma
hivyo mali nyingi za walala hoi zinataifishwa kutokana na kutoelewa kwa mkata
husika ama kushindwa kulipa riba ambayo amewekewa,Alisema Flaviana
Naye kwa upande wake meneja mradi wa kazi za staha kwa
wananchi waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi, Bw.Hussein Sengu amebainisha
changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakikumbana nazo katika utekelezaji wa
mradi huo uliofadhiliwa na umoja wa Ulaya (EU) ambapo katika kazi hiyo
walishirikiana kwa karibu na shilika la kijerumani linalohuska na idadi ya watu
ulimwenguni Deutsche stiftung weltbevoelkerung (DSW) , kuwa matatizo makubwa ni
vilio vya wajasiliamali ambao wamekuwa wakitapeliwa mali zao na kuacha makazi
yao huku serikali likifumbia macho suala hilo.
Unakuta watu wanakufuata kwa upendo kabisa kuwa kunapesa
lakini, mwisho wa siku ni vilo kwani masharti ni magumu na yasiotekelezeka
hatua inayowafanya watu wengi kupoteza mali zao za thamani kwa pesa ndogo
waliochukua kujianzishia biashara wenyewe,
Taasisi ya ujasiliamali inaajiri takribani asilimia 60 ya
watanzania wote, hivyo kitendo cha kuacha tasnia ya ujasiliamali kuwa haina
mwenyewe ni hatari kwa mustakali wa taifa letu, Aliongeza Sengu wakati
akifafanua utapeli unaofanywa na mashirika ya kukopehs afedha kwa wajasiliamali
.
HAYA NDIYO MAPENDEKEZO YA KITUO KAMA KWELI TUNATAKA
KUWANASUA WAJASILIAMALI:
·
Serikali iunde mamlaka ya kudhibiti tasnia ya
ujasiliamali, kwa kuzidhibi taasisi za mikopo isiende nje ya sera ya mamlaka itakayoundwa
·
Watunga sera watunge sra zitakazoweka misingi ya
sekta sisizo rasmi
·
Serikali ijipime na kuanza kuangalia sekta ya
ujasiliamali na kuweka mifumo ili kuondoa dhuluma, wizi na utapeli unaoanza
kukua kama uyoga katika taasisi za kukopesha fedha
MWISHOO
Maoni 1
Hii ni muhimu kabisa kwani wajasiriamali wa najaribu kujikwamua kiuchumi wakati wakichangi apat la taifa , nguvu zao hupotea iwapo watatapeliwa.
HELEN
Chapisha Maoni