Zinazobamba

ATHARI ZA UKAWA ZAANZA KUTIKISA NCHI, UMOJA WA ASASI ZA KIRAIA WATAKA BUNGE LIVUNJWE


Mwenyekiti wa asasi zisizo za kiserikali Bw.Irinei Kiria, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari juu ya Tathimini  zilizofanywa na asasi za kiraia kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba mpya unaoendelea katika bunge la katiba mjini Dodoma,Katika tahimini yao hiyo, umoja huo umegundua madhaifu mengi sana ambayo kama hayatapatia ufumbuzi wake basi katiba mpya yenye kumjali mtanzania ni Ndoto kupatikana.

Deusi Kibamba mmoja wa wanachama wa ummoja huo wa asasi zisizo za kiserikali akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya athari za wabunge kutoka bungeni huku wengine wakiendelea kujadili katiba hiyo, Kibamba amesema, kisheria katiba lazima iwe ya makubaliano, na kama katiba inaendeshwa kibabe basi katiba hiyo si ya wananchi bali inawakisha kundi fulani yenye maslahi binafsi. Kibamba ameshauri bunge hilo livunjwe kwani mpaka sasa lionesha dalili zote kupendelea maslahi ya kundi fulani na si ya mtanzania ambayo rasimu ya katiba imependekeza., Kuanza upya si dhambi.
Siku moja baada ya baadhi ya wajumbe wa bunge maalum la katiba (UKAWA) Kusuia shughuli za bunge maalum la katiba wakidai bunge hilo kuendeshwa kibabe na kuzingira kwa vitisho mbalimbali kutoka kwa selikali, Umoja wa asasi za kiraia hapa nchini umetafsiri hatua hiyo kuwa ni ya kishujaa na inayolenga kumpatia mtanzania katiba anayoitaka na siyo katiba yenye kufaidisha  kundi fulani,

Wakizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, umoja huo unaounganisha zaidi ya asasi 500 toka mikoa mbalimbali ya nzi yetu, wamesema hatua ya wajumbe kutoka katika bunge hilo la katiba inaonyesha wazi ni kwa jinsi gani katika bunge hilo hakuna maridhiano miongoni mwa wajumbe,na kuongeza kuwa kama hakuna maridhiano katika kuandika katiba ya kuliongoza taifa hili kwa miaka mingine 50 haitawezekana,
Wameongeza kusema kuwa, katiba yeyote duniani inayoandikwa ni lazima kuwe na makubaliano, sasa inapokuja suala la kutokuwepo kwa makubaliano miongoni mwa wajumbe, katiba hiyo haitakuwa na maana kwa wananchi,

Unakuta kundi, fulani linatumia wingi wao kushinikiza jambo wanalotaka litokee, sasa huo sio maridhiano na badala yake ni kulazimishana, kitu ambacho si halali,
Katika hatua nyingine Umoja huo umetoa angalizo kwa watu wanaolazimisha, malengo ya makundi yao yapite na kuacha nyuma malengo ya watanzania walio wengi, na kusema kuwa hatakama watafanikiwa kupitisha, katiba hiyo itakuwa si ya watanzania wote bali ni ya kundi fulani yenye maslahi nayo,

Aidha umoja huo umependekeza bunge hilo kuvunjwa mara moja ili wananchi wapate fulsa ya kuanza na moja kwani bunge hilo kwa sasa limeonyesha, kushinda kutafuta katiba na badala yake limejikita katika kutoleana lugha za kejeli, matusi na na kuvunjiana heshima, suala ambalo halikuwapeleka hapo.



Katika tahimini ambazo asasi za kiraia wamefanya juu ya mwenendo wa bunge la katiba, umegundua kuwa kuna dalili ya kupatikana kwa katiba ya kundi fulani, hivyo wameakuja na muarobani wa tatizo hilo kwa kutoa mapendekezo ambayo yakifanyiwa kazi basi katiba ya watanzania wanayoitaka itapatikana na vinginevyo, basi tutarajie katiba ya watu fulani, na haya hapa ndio maoni yao

  • wanaunga mkono rasimu ya pili ya katiba kama ilivyowasilishwa na jaji walioba,
  • wanasikitishwa kwa namna mijadala inavyoendeshwa kihuni, mijadala iliyopoteza utaifa, na iliyojikita katika matusi na kuvunjiana heshima,
  • wanasikitishwa kwa hatua ya kudhihaki rasmu ya pili ya katiba ya jaji walioba ambayo ndio maoni hali ya wananchi,
  • Wamesikitishwa na maoni ya kutaka kuondoa tunu ya taifa ya maneno uwajibikaji, uwazji na uwadilifu, wanaogopa nini?
  • hatua ya kuruhusu wabunge wa kuchaguliwa kuingia bunge la katiba tumekosea sana, huwezi kumwajibisha umempa makali, lazima atajipendelea
  • Malumbano yasiyo ya tija , yamewasikitisha sana,
  • kufungwa kwa tovuti ya walioba imetuuma sana, fungueni , kwani tunaogopa nini jamani, wamesema.

Maoni 3

Bila jina alisema ...

katiba ni jambo la maridhiano,UKAWA kutoka nje ya Bunge ni ishara ya kutokuwa na maridhiano.czan kama wajumbe waliobaki wanaweza kuleta katiba iliyo bora kwa sababu haina maridhiano...tujaribu kuangalia suala hili kwa makini.....rais fanya maamuzi magumu ya kuvunja bunge la katiba na kufikiria namna mpya ya kupata katiba ya wananchi.

Bila jina alisema ...

Bwana Musiwababaishe Wazanzibari, Katiba inayotungwa ni ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hilo haliepukiki.. Sasa hilo Taifa linakuja baada ya Nationality za Nchi mbili hizo zilizounda Muungano... kama watanganyika Wanakataa Historia yao ya Tanganyika mabyo ina kila kitu chakujivunia.. Basi Wazanzibari hawapotezi Identity yao kama Wazanzibari... Serikali 3 ni njia ya kuona mbele na Muungano unatakiwa uwepo hapo kwakuunganisha Nchi hizo na Raia wake.... Hili suala la Benard Membe kuja na hoja kwamba Serikali 3 zitakua hazina maana kwasababu zitakua hazina Nguvu huo ni Uamuzi wa hao CCM waliozoea Vyakunyonga... Miaka yote 50 Wazanbzibari wamekua wakigaiwa tonge kama mtoto yatima.. Na hivo tunasumbuliwa na kutukanwa... Kukashifiwa .. Ukweli Wazanzibari hawataki kutawaliwa na Wakoloni WEUSI .. Ni bora utawaliwe na Mkoloni Mweupe atakunyima baadhi ya mambo tu lakini ukiwa na ujuzi wa kazi na elimu hawezio kukubagua.. kuliko Nyinyi Watanganyika.. hasa wale CCM.. Ni wakorofi sana .. Tumechoka kuiona CCM inatumia Rasilimali za Muungano kwa shuhuli za Kichama... Chama kinatakiwa kiwe na vyanzo vyake vya mapato..... Mbona Chadema, CUF au DP hawatumii hela ya ST... ?

Bila jina alisema ...

@ Ananymous 2
Maneno yako ni sawa kabisa lakini CCM wanaotumia Rasilimali za Serikali ya Muungano kwa Shuguli za Kichama ni CCM wanaotoka Bara.. Hivi leo nilisoma www.zanzinews.org nikaona Yule Mnafiki wa KINANA nafungua Mradi wa Kujenga nyumba za mkopo nafuu huko katika Vijiji vya Tanganyika... Na Nyumba hizo za Mikopo nafuu zimeshajengwa sehemu Nyingi sana za Huko Tanganyika...... Wale CCM wa Zanzibar wamo kama Madubu tu wanapopewa hela ya Chama kwanza hugaiwa kidogo sana na nikwaajili yakufungulia Matawi.. Kununulia Risasi zakuwauwa Viongozi wa Dini Zanzibar au zakujengea Makanisa... Kwa upande wa Visiwani CCM inaimarisha mambo 3 makubwa:
1. Makanisa.
2. Maskani za CCM katika Mitaro ya Maji na Sehemu za Wazi.
3 Kuwapatia Suilaha Janjawee kwaajili yakuhujumu wananchi.

Kwa Upande wa Tanganyika CCM wanachota hela ya Muungano kwaajili yakujengea Barabara utafikiri hakuna waziri anaeshuhulika na Ujenzi ao Miuondo Mbinu.. Kujenga Magati n.k.. Na ndio maana wanataka serikali 2 ili Waendelee kuwadhulumu Wazanzibari na Vyama vya Upinzani Tanganyika..