WAKULIMA HAWATAPONA,
Katika kile kinachoonekana kushindwa kwa wakala wa serikali wa vipimo kutekeleza majukumu yake ya kuondoa kero ya matumizi ya vipimo visivyo rasmi kwa wafanyabiashara hapa nchini, hatua hiyo inatafsriwa kuwa sasa wakulima hawatapona dhidi ya dhuluma wanayotendewa, Fullhabali inashuka nayo
Wakala wa vipimo ambao wamepewa dhamana ya kusimamia suala zima la vipimo hapa nchini, wameamua kuja na mikakati mipya ya kuchota fedha za umma kwa staili ya aina yake ya kufanya tafiti huku wakiacha tatizo la matumizi ya madebe yakiwatafuna wakulima
Mtandao huu umefanya utafiti wa kina na kubaini kuwa wakala wa vipimo wameanzisha mchakato wa kufanya utafiti juu ya matumizi ya vipimo visivyo rasmi hapa nchini wakitumia jumla ya mikoa mitano, Huku wakijua wazi kuwa tatitzo la matumizi ya vipimo visivyo rasmi lipo toka zamani,
Wakizungumza na Mtandao huu, baadhi ya wakazi wa jiji la Daresaalam, wamesema Tatizo la matumizi ya Lumbesa, madebe na visado wala halihitaji tafiti, ukizingatia kuwa matumizi ya vipimo hivyo wala hayajifichi hata ukienda buguruni utagundua uwepo wa tatizo hilo
Katika hali isiyotarajiwa,Wakala Wa Vipimo wa serikali WMA wameamua kufanya tafiti na kuja na wimbo uleule wa uwepo wa tatizo la matumizi ya vipimo visivyo rasmi, huku tafiti hizo zikitafuna mamilioni ya shilingi, kodi za mlala hoi, huku wakijua wazi kuwa tatizo hilo lipo na kwa kiasi kikubwa, hatua iliyotafsiriwa kuwa ni matumizi mabaya ya rasimali za umma kwa wakala hao wa serikali,
Uchunguzi unaonyesha kuwa, Hivi karibuni wakiwa wanaongea na waandishi wa habari, viongozi wa wakala wa serikali wakiwa wameambatana na afisa habari wao mkuu Bi. Irine John, walisema wazi kuwa tatizo la matumizi ya madebe, Lumbesa, Visadolini bado limeshamili sana hasa maeneo ya buguruni na mikoa ambayo wamefanyia utafiti
Watafiti wa mambo wanasema,hawakushangwaza kabisa na majibu ya utafiti huo lakini kinachowashangaza wao ni kwamba kwani tokea awali wanapanga mkakati wa kufanya tafiti walikuwa hawajui kama tatizo hilo lipo tena kwa kiasi kikubwa ama ndio wimbo uleule kuwa kulikuwa na ajenda ya siri kufanya tafiti ambayo tayari yanamajibu yake
Nashawishika kusema kuwa wakala wa vipimo hawana nia ya dhati kumnusuru mlala hoi anayepata hasara kila leo kwa kununua bidhaa pungufu huku wafanyabiashara wakiendelea kuuneemeka kwa matumizi ya vipimo hivyo, aliongeza mmoja wa msomi maarufu hapa nchini ambae hakutaka kutajwa jina lake hapa mtandaoni
Ikumbukwe kuwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara , Joyce Mapunjo, wakati akifungua warsha ya matumizi sahihi ya vipimo na viwango aliwahi kunukuliwa akisema utafiti wa matumizi ya vipimo visivyo rasmi unaonyesha kutapakaa kwa kasi ya ajabu matumizi ya vipimo visivyo rasmi.
Akiwa katika Warsha ya kuzindua tafiti za namna wafanyabiashara wanavyotumia lumbesa kumnyonya mkulima, huku wafanyabiashara hao wakitumia vipimo visivyo rasmi kumnyonya mlaji,Mapunjo alisema hatua hiyo haikubaliki na lazima hatua za haraka zichukuliwe kuondoa tatizo hilo,
Katika warsha hiyo iliyoandaliwa na muungano wa Asasi ya Tanzania Markets Policy Action Nodes (TM-PAN) na kufadhiliwa na Shirika la Alliance for Green Revolution in Africa (AGRA) katibu huyo hakusita kuonyesha kukerwa kwake kwa matumizi ya Lumbesa madebe pamoja na visado .
Katika warsha hiyo ambayo tafiti za vipimo visivyo rasmi zilikuwa zikiwasilishwa, mtafiti kutoka Shirika la MRA Associates, Charles Ogutu, alisema utafiti umebaini kuwa bado hakuna mfumo unaoeleweka unaodhibiti matumizi sahihi ya vipimo na viwango.
Alisema miongozo mingi na kanuni imeandikwa kwa lugha isiyoeleweka kwa mkulima wa kawaida. Alisema katika utafiti huo, wamebaini kodi za mazao na masoko zinatozwa kulingana na idadi ya magunia badala ya uzito hivyo inatoa mwanya kwa wafanyabiashara kujaza lumbesa. Alisema utafiti umeonyesha kuwa taasisi za kiserikali kama WMA, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) vina idadi ndogo ya rasilimali watu.
UKUBWA WA TATIZO
VILIO VYATAWALA IRINGA
Ikumbukwe kuwa mwaka jana sauti ya mlala hoi toka mkoani Iringa katika Kijiji cha Lumuli, wilayani Iringa walitoa machozi na kuiomba Serikali kuwasaidia kusimamia vipimo vya mazao yao wakati wa uuzaji ili wasilanguliwe na wafanyabiashara wakubwa wanaotumia lumbesa, madebe na visado kilio ambacho mpaka leo hakijapata msikilizaji.
Wanakijiji hao waliwahi kumpigia magoti mkuu wa mkoa huo enzi hizo,Dk Christine Ishengoma wakimtaka aingilie kati suala hilo la unyonyaji, lakini wapi mpaka leo, bado mazao yao yanauzwa kwa lumbesa kama tafiti mbalimbali zinavyoonyesha,.
Akitoa kilio chao, Kwa mkuu wa mkoa huo wa Iringa Enzi hizo, mkazi wa
kijiji hicho Silvester Mwinuka alinukuliwa akisema wanakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwamo kulanguliwa na wafanyabiashara wakuwa kwa kupima viazi
kwa ujazo wa ‘Lumbesa’.
Aidha alibainisha sababu za wao kulazimika kupima lumbesa ni kutokana na kukosa soko la uhakika la kuuza viazi vyao hatua inayowalazimisha kupima mazao yao kupitia vipimo visivyo rasmi la sivyo mazao hayo yataozea shambani huku wakidaiwa pembejeo walizotumia ,kuzalisha mazao hayo
Hata hivyo alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo na sheria inasema nini, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa
Vijijini, wa enzi hizo Pudenciana Kisaka alisema, sheria ya kuzuia Lumbesa ipo na
kuongeza hata kwenye vizuizi ujazo wa ‘Lumbesa’ huzuiliwa. Sasa swali la kujiuliza ni kwamba wanampango gani na huyu malala hoi, ambae kila kukicha anaambiawa kilimo kwanza, kilimo kwanza, kilimo kwanza kiko wapi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni