Zinazobamba

WAKAGUZI WA NDANI UCHAGUZI WA KALENGA WATOA TAHMINI YAO, WASEMA UCHAGUZI ULIGUBIKWA NA VITENDO VYA KIKATILI,VITISHO, UBAGUZI WA KIJINSIA,... WAITAKA NEC KUJIPANGA KABLA YA CHAGUZI

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu, Wakili Imelda Lulu Urio akifafanjambo mbele ya waandishi wa habari, ulio alisema kwa kauli moja wanaalani vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na udhalilishaji wa haki z binadamu uliofanywa na wafuasi wa chama cha Chadema na CCM katika uchaguzi huko jimboni Kalenga. Picha kwa msaada wa Habari24

Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania LHRC kwakushirikiana na mtandao wa mtandao wa taasisi zisizo za kiserikali kusini mwa Africa SAHRINGON kimetoa tathmini yake juu ya mchakato mzima wa uchaguzi katika jimbo la kalenga huku tahimini hiyo ikionyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi wa kijisia 

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam wakili EMELDA URIO ambaye ni kaimu mkurugenzi mtendaji wa LHRC pamoja na MARTINA KABISAMA ambaye ni mratibu taifa wa SAHRINGON wamesema kuwa katika kampeni za uchaguzi huo kituo chao kilishughudia uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi wa kijinsia kwa wagombea wa jinsia ya kike jambo ambalo wamesema ni kinyume na sheria za uchaguzi wa Tanzania.


 Wamesema kuwa moja ya udhalilishaji mkubwa uliofanywa na viongozi katika kampeni ni naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara MWIGURU NCHEMBA alipotoa kashifa nzito dhidi ya wabunge wanawake wa chadema akidai kuwa wabunge hao wanatumika kingono hatua waliyosema ililenga kumzalilisha mwanamke wa kitanzania
Viongozi hao walisema Nchemba alinukuliwa katika kampeni za CCM mkutano wa tarehe 15 mwezi wa 3 akisema kuwa wabunge wa viti maalum wa CHADEMA wapo bungeni kwa ajili ya kuwahudumia wabunge wa CHEDEMA wanaume kingono hivyo akawataka wananchi wa kalenga kutokumchagua mgombea wa chadema GRACE TENDEGA kwani naye ataenda kufanya hivyo kama atafanikiwa kuingia bungeni.

    KABISAMA amesema kauli kama hizo ni za kidhalilishaji na za kuwanyongonyesha wanawake kwa ujumla na kukemea kauli kama hizi kwa ni zinaondoa heshima na utu wa wanawake.

Katika uchaguzi huo vitendo vya uvunjifu wa usalama ulishamili hasa kitendo cha kukamatwa na kutekwa kwa mbunge wa chadema Mh. Rose Kamili na kupigwa na wafuasi wa chama cha mapinduzi CCM huko kalenga wakimtuhumu kuhonga wapiga kura

Hakuna maoni