WADAU WA REDIO JAMII WASEMA YA MOYONI, SIDA ,UNESCO YAPONGEZWA
MAWAKALA WA REDIO JAMII WATAJA FAIDA ZA MRADI WA SIDA PANGANI
Afisa
Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph, akisisitiza jambo katika warsha ya siku tatu ya kutoa uwezo wa
kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa kutumia Teknolojia
mpya.
Na. mwandishi wetu, Pangani
Mawakala
wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo mbalimbali yanayofadhiliwa na
Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kushirikiana na Shirika la
Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) wametaja mafanikio waliyoyapata kutokana na mradi unaotoa uwezo
wa matumizi wa tehema katika redio jamii katika upashaji wa habari .
Wakitoa
tathmini ya maendeleo ya mradi katika warsha inayowapa uwezo wa kuweka
kumbukumbu za kazi zao na vyanzo vya habari kwa kutumia Tehama
iliyofanyika Pangani, washiriki hao wamesema mafanikio hayo siyo tu
katika taaluma bali pia yamewajenga na kuwaimarisha kimaisha.
Mmoja
wa washiriki hao alisema, “kusema ukweli natoa shukrani zangu kwa SIDA
na UNESCO kwa kutupatia mafunzo haya kwa sababu mimi binafsi nimeweza
kununua kompyuta pakato (laptop) kwa ajili ya kuendeleza niliyoyapa
kwa vitendo, na niko mbioni kununua simu za kisasa aina ya ‘tablet’,”
alisema Sospether Rugemarila kutoka Fadeco FM redio.
Sehemu ya washiriki wakifutilia kwa umakini mafunzo hayo.
Katika
kipindi cha miaka miwili cha mradi huo, mafunzo mbalimbali yametolewa
kwa mawakala wa redio jamii kama vile matumizi ya mtandao katika
kutafuta habari, mbinu mbalimbali za kupeleka taarifa na vipindi vya
redio kupitia mtandao, matumizi ya simu aina ya ‘smartphone’ katika
kuripoti taarifa maalum au majanga na matumizi ya mitandano ya kijamii
kwa lengo la kuwasiliana, kushirikiana na kubadilishana mawazo, taarifa
na vipindi vya redio.
“Sisi
baada ya kupata mafunzo ya matumizi ya simu aina ya “smartphone”
tulifungua akaunti ya pamoja ya Facebook kwa jina na UMMAREJA kama
ulingo wetu wa kubadilishana mawazo, taarifa na masuala mbalimbali
yanayohusu ustawi wetu kama mawakala,” alisema mwenyekiti wa umoja huo
Msuli Mwaijengo kutoka Kyela FM redio.
Sospeter
Rugemarila wa FADECO FM Redio, akizungumzia mafanikio aliyoyapata
kutokana na mafunzo ya kuzipa uwezo Redio Jamii matumizi ya Teknolojia
mpya katika kukuza upatikanaji na upashaji habari vijijini.
Sabina
Nestory ni miongoni mwa mawakala ambao walikuwa na uwezo mdogo sana
kabla ya mafunzo haya kuanza. Lakini ila anapohudhuria mafunzo mapya na
kiwango chake pia kimekuwa kikiongezeka kiasi cha kumfanya aone umuhimu
wa kununua simu aina ya ‘smartphone’ ambayo anasema itamrahirishia
kutafuta na kutuma taarifa mbalimbali kwa niaba ya chama cha Umoja wa
Wanawake katika Habari na Mawasiliano Sengerema (WAHAMASE) unaomiliki
kituo cha Sengerema FM redio.
“Mimi
nilipohudhuria mafunzo ya Tehama Ifakara nilikwenda moja kwa moja
dukani kununua simu ya ‘smartphone’ ili nione inafanyaje kazi, ninayo,
bado naisoma huku nikiendelea kuitumia kwa kuripoti matukio mbalimbali
ya vijijini hususan ya maendeleo”.
Peter
Marlesa wa Sengerema FM Redio, akielezea jinsi alivyofanikisha
kutayarisha makala na vipindi mbalimbali zikiwemo habari za Mahakama na
migogoro vijijini.
Mafunzo
hayo yameweza kuwapandisha ngazi baadhi ya mawakala kuwa wafanyakazi
vituoni baada ya kuonyesha umahiri na ujasiri katika utekelezaji wa
majukumu ya kila siku kama ilivyofanyika Mtegani FM redio, Makunduchi
Zanzibar na Sengerema FM, Sengerema Mwanza. Peter Marlesa ni miongoni
mwa waliobahatika kupanda ngazi kutokana na umahiri na ubunifu wake
katika kuandaa vipindi mbalimbali kwa kujituma.
“Baadhi ya mambo niliyofaidika na mradi ni utayarishaji wa vipindi vya
makala ya redio, jarida, vipindi vinavyohusu makundi maalum, habari za
mahakamani na migogoro na taarifa za habari. Ni mara ya kwanza katika
kituo chetu kuandika habari za mahakamani na maeneo tata vijijini.”
Kwa
mara ya kwanza warsha hii ya kuwapa uwezo wa kuweka kumbukumbu
imewakutanisha mawakala 25 kutoka redio tisa ambazo ziko kwenye mradi wa
kuzipa uwezo redio jamii matumizi ya Tehama ulioanza mwaka 2012 ambao
baada ya hitimisho watapitiwa vyeti vya ushiriki. Redio hizo ni Fadeco,
Kahama, Kyela, Micheweni, Mtegani, Orkonerei, Pambazuko, Pangani na
Sengerema.
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa maelekezo jinsi ya kufanya mazoezi kwa vitendo.
Sabina
Nestory wa Sengerema FM Redio, akionyesha Smart Phone yake aliyoinunua
wakati wa mafunzo ili kufanikisha mafunzo ya matumizi ya simu na habari
kwa vitendo.
Afisa
Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama kutoka UNESCO, Bw. Al
Amin Yusuph, akiewaelekeza jambo washiriki namna ya kuhifadhi habari
kwa kutumia simu yenye uwezo mkubwa (Tablet).
Programme
Assistant wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka UNESCO, Rosemary
Lyamba, akitoa maelekezo kwa washiriki katika warsha ya siku tatu ya
kutoa uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa
kutumia Teknolojia mpya iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden
(SIDA) wa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia
masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Picha juu na chini ni washiriki wa warsha hiyo wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Teknolojia mpya ya TABLET.
Washiriki wakiwa kwenye kazi za vikundi.
Mshauri
na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu akiwa
kwenye picha ya pamoja na mawakala wa Redio Jamii nchini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni