|
Posta
masta mkuu na mtendaji mkuu wa shirika la posta Tanzania, akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa mpango kabambe wa
miaka kumi wa shirika la posta Tanzania, Mpango huo unatarajiwa
kukamilika kwakwe 2023 ambapo shirika hilo litaweza kutoa huduma bora
ambayo yenye kiwango cha kimataifa ukilinganisha na sasa |
Wakati Tanzania inaelekea kuazimisha miaka hamsini ya muungano,shirika la posta Tanzania limeanza tekelezaji wa mpango kabambe wa miaka kumi ikiwa ni dira na mwelekeo wa kuliongoza shirika hili liweze kujiendesha kibiashara, kubuni na kutoa huduma mbadala, kutumia teknolojia maridhawa na kukidhi mahitaji ya soko ya huduma ya mawasiliano jumuishi,
Akizungumza na waandishi wa habarimapema hii leo jijini Daresaalam, Posta masta mkuu na mtendaji mkuu wa shirika hilo amesema shirika limeanza utekelezaji wa mpango huo wa miaka kumi ulioanza mwaka huu na kukamilika kwake 2023 ili kuweza kuboresha huduma za shirika pamoja na kuharakisha jitihada za serikali ya kufanya taifa kuwa la kipato cha kati
|
Mwandishi mwandamizi, Akiwa makini kuchukua taarifa inayotolewa na mkurugenzi mtendaji huyo mapema hii leo, Mkurugenzi amewahakikishia watanzania kuwa hhuduma bora ya usafiri wa vifurushi na barua itakuwa ya kiwango cha juu kiasi cha kuwavutia wateja wengi kujiunga na huduma inayotolewa na shirika hilo, Ambapo kwa sasa takwimu zinaonyesha kuwa wananchi wengi hawafaidi huduma za shirika la posta . |
|
Posta masta mkuu akisikiliza mapendekezo ya waandishi wa habari ju ya kuondoa kero za ucheleweshaji wa barua zinazotumwa kupitia masanduku ya barua ya shirika la posta,Mkuu huyo amesema changamoto kubwa inayowakabili shirika hilo ni kwa wananchi kutumia sanduku moja kwa wateja zaidi ya elf moja, sasa unakuta mtu barua yake haipati kwa wakati sababu tu mwenye funguo hajaenda kuangalia katika sanduku lake, amesema sasa kuondoa kero hiyo wamejipanga vema kwa kuanzisha mpango wa kitaifa ambapo kila mwananchi atafahamika eneo analotoka hivyo kuwa rahisi kufikishiwa barua yake |
|
Kaimu
meneja biashara, Bw.Jasson Kalille akifafanua jambo juu ya hatua
iliyofikiwa kwa shirika hilo kuanza kuipanga mitaa kwa kuweka kodi za
kata vijiji na hata mitaa, ambapo Meneja huyo amesema kazi imeshaanza na
kwamba mikoa ya Arusha na Dodoma mambo yanaenda vizuri huku Katika jiji
La Daresalaam wamefanikiwa kufanya hivyo kwa kata kumi ambapo Ilala ni
kata nne, temeke tatu na kinondoni kata tatu, |
|
Pichani kulia ni meja mkuu uendeshaji wa Biashara, Fortunatus Fortunatus Kapinga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari juu ya mpango kabambe wa miaka kumi wa shirika hilo la posta, Meneja huyo amesema shirika hilo limejipanga kuanza kujiendesha kibiashara na kubuni nzia nzuri ya kuwahudumia watanzania kwa kukabiliana na changamoto ambazo zinaonekana kulikabili shirika |
|
Posta masta mkuu akijibu moja za hoja za waandishi wa habari katika mkutano wake na waandishi wa habari |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni