kukamatwa kwa wachina na meno ya Tembo, Balozi Lu afafanua, ..., pia atoa ufafanuzi kwa nini bidhaa za china zinaunekana ni bidhaa mbovu katika macho ya watanzania,
Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje Mh. John Haule akifafanua baadhi ya hoja za waandishi wa habari walikuwa wakitaka kujua biashara ya meno ya tembo na china kulikoni????, Haule am,ewatoa wasiwasi watanzania kuwa biashara ya meno ya tembo haikubaliki hata huko china |
Na Magari, Maelezo
WIZI WA MENO YA TEMBO, WACHINA WAFAFANUA
Kuafuatia matukio mbalimbali yaliwahusisha raia wanchi ya
china dhidi ya biashara ya meno ya tembo, Balozi wan chi hiyo hapa nchini
ameibuka na kuweka mambo hadharani kwa kusema kuwa wachina wamesikitishwa na
vitendo hivyo vya raia wake na kwamba walikuwa watu wa kwanza kuomba msamaha
juu ya tukio hilo,
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii mleo jijini
Daresalaam,Balozi wa nchi ya china hapa nchini, Dr Lu youqng matukio hayo kwa kiasi kikubwa yamewachafua
tabia njema ya wachina na kwamba, kama nchi walionyesha juhudi zote za kusaidia
kudhibiti biashara hiyo haramu ya meno ya Tembo kwenda nchini China,
Balozi Lu, ameongeza kusema kuwa, tayari serikali yake
imeshatoa dhana zitakazosaidia kutambua majangiri wa meno ya tembo kwani biashara hiyo hakika haikubaliki kuendelea
kuiendesha,
Akizungumzia suala la sheria za china dhidi ya makosa ya
jinai kwa wahalifu wanaokamatwa toka nchini Tanzania, Balozi Lu, amesema kwa
kiasi kikubwa watanzania ambao wamekamatwa kwa biashara haramu huko china,
hawajanyongwa na kwamba wale wote waliokamatwa bado wapo katika magereza yao
wakisubiria hukumu yao ya kifungo cha maisha kama sheria ya nchini mwao
inavyosema.
Akijibu swali la mwandishi mwandamizi wa Mtandao pendwa wa
fullhabari, kuhusiana na hatua zinazochukuliwa dhidi ya wachina wanaokamatwa na
meno ya tembo hapa nchini, balozi Lu amesema wachgina hao wanahukumia kama raia
wengine wanaotenda makosa ya jinai,
Aidha katika hatua nyingine, Balozi Lu amewataka
wafanyabiashara hasa wa kichina kuongeza ubora wa bidhaa wanazoziuza katika
nchi ya Tanzania ili kuwafanya wateja wa kitanzania kufaidi huduma bora na
uhakika,
Lu amesema kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusiana na
ubora wa bidhaa za kichina, ambalo kwa kiasi kikubwa imekuwa kero nkubwa sana
kwa watanzania hivyo ameamua kuwataka waagizaji wa bidhaa hizo kuagiza bidhaa
zinazokidhi viwango vya kimataifa ili kumuondolea mteja hasara isiyo ya
lazima.,
Naye kwa upande wake Katibu mkuu wa wizara ya mambo nje hapa
nchini, Mh.John Haule amewataka mashirika yanayojihusihsa na ubora wa bidhaa
kuwajiobika ili kumlinda mteja na bidhaa zinazokosa ubora katika ardhi ya
Tanzania
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini |
Amesema kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusiana na
bidhaa za kichina lakini bado mamlaka husika hazitoi ufafanuzi sasa hii sio
Tatizo la wachina bali ni tatizo la watanzanaia wenyewe ambao taasisi zetu
zinaruhusu kuingia kwa bidhaa ambazo hazina ubora,
Unakuta watu wanajiunga wakiwa makundi wanaenda china
wananunua mzigo, ambao hakika hauna viwango lakini ukifika bvandarini bado
unaruhusiwa kupita harafu lawama wanapewa wachina, hiyo si haki hata kidogo
aliongeza Mh. Haule
Aidha katika hatua nyingine Katibu mkuu huyo wa wizara ya
mambo ya nje amefafanua juu ya dhana ya wachina kufungua viwanda katikati ya
makazi huku wakiwa hawana vibari kuwa ni uzembe wa mamlka zetu ,
Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo akiwakarisha wachina katika ukumbi huo. |
Amesema si kweli kuwa wachina hawaonekani wakiwa wanafunzua
hivyo viwanda, watu wapo wanawaona lakini wanakuwa kimya hadi wananchi
walalamike ndipo wachukue hatu,
Mambo mengine huwezi kumlaumu mchina, wewe kama mtanzania
umefanya nini kumuwezesha huyu mchina anaefungua viwanda katika makazi ya watu,
kwani tukiweza kuwapangia maeneo kero hizi za kufungua viwanda katikati ya
makazi ya watu hazitakuwapo hata kidogo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni