Jakwaa la katiba lafafanua mwenendo wa bunge la katiba mjini dodoma, yasema wasipojirekebisha watatumia nguvu ya umma kulifunga bunge hilo
Kaimu mwenyekiti wa jukwaa la katiba Hebroni Mwakagenda, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari. Mwakagenda amesema hali ikiendelea hivi ya zomeazomea, hawatasita kuwaomba wananchi kulifunga bunge hilo kwani linatumia kodi zetu vibaya |
Jukwaa la katiba limewataka wajumbe wa bunge la katiba kujitazama upya na kuchukua hatua za haraka kuacha mienendo mibaya na inayoleta hasira kwa wananchi wanaolizama bunge hilo, ambalo limezingirwa na zomea zomea pamoja na kuhairishwa kwa vikao harali mara kwa mara, Vinginevyo watakwenda dodoma kulifunga bunge hilo
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, Makamu mwenyekiti wa jukwaa la katiba haba nchini, Mh.Hebron Mwakagenda, amesema hatua hiyo imekuja kufuatia zomea zomea ambayo imelikumba bunge hilo tokea limeanza pamoja na kuahairishwa kwa vikao muhimu, huku wakijua wazi kuwa wanatumia mamilioni ya shilingi toka kwa mtanzania mlala hoi,
Mwakagenda amesema, mpaka sasa bunge hilo limekuwa likitumia mamilioni ya shilingi ambayo hawayafanyii kazi,hatua iliyotafsriwa ni unyonyaji wa kodi ya mkulima ambaye anataka kuona katiba bora yenye kujali maslahi yake inapatikana tena kwa wakati
Mwakagenda ameongeza kusema kuwa, tokea kuanza kwake kwa bunge hilo la katiba kumekuwa na mwenendo ambao haurizishi kwa watazamaji yeyote yule anaeangalia bunge hilo, hasa mfano tukio lile la tarehe 17/03/2014 saa kkumi jioni ambapo bunge hilo lilivunja kikao baada ya kuwa na ubishi usio na tija,
Amesema hata hoja ya eti kwanza aanz raisi ndipo asome mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, Mh. JOSEPH Sinde Walioba ilikuwa haina mashiko kwani mbona siku ya pili yake walikubali kusomwa kwa hutuba hiyo ya sinde Walioba? alihoji Mh. Mwakagenda
Bunge hilo linatarajiwa kuendelea hapo kesho kwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kurihutubia bunge, inatarajiwa kuwa rais ataambatana na marais waastaafu, pamoja na viongoz wastaafu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni