SERIIKALI YAKUSANYA MABILIONI YA SHILINGI KUPITIA MPANGO WA BIG RESULTS NOW, MABLOGGERS WAPEWA SEMINA
Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
|
Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now). |
Haya yamo katika taarifa aliyoitoa
msemaji mkuu wa wizara ya Fedha Bi alipokuwa akitoa taarifa ya utaratibu
huo kwa wanablogu, katika kikao maalum na wadau hao kilichofanyika nje
kidogo ya mkoa wa Pwani, maeneo ya Misugusugu.
Bi Mduma alisema Wizara ya Fedha ni
miongoni mwa Sekta zinazotekeleza utaratibu huu hususan katika eneo la
utafutaji wa mapato (Resource mobilization), sekta nyingine ni Elimu,
Kilimo, Maji, Uchukuzi na Nishati.
Utekelezaji wa kila sekta unazingatia
viashiria vilivyoibuliwa katika uchambuzi wa kimaabara ulioratibiwa na
Serikali kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Malaysia.
Alisema huu unaiwezesha Serikali
kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo
usimamiaji wa miradi kwa kuweka wazi malengo yaliyokusudiwa pamoja na
kuainisha viashiria vya utekelezaji ili kuongeza uwajibikaji kwa kila
mshiriki.
Aidha, viashiria hivi hutumika kupima
hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maeneo ya kipaumbele na hivyo
kuweza kupima mafanikio yaliyopatikana. Kadhalika, utaratibu huu
unasaidia kurekebisha mapungufu katika utekelezaji kwa kuchukua hatua
mapema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa matokeo makubwa kwa haraka.
Bi Mduma amesema wizara yake imedhamirisa utafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16;
Hakuna maoni
Chapisha Maoni